Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza
Mwamlima amezindua rasmi
Baraza la Biashara la Wilaya ya Mpanda lenye lengo la kuwaunganisha wafanyabiashara
na Serikali
Mwamlima alizindua baraza hilo la biashara hapo jana katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ulioko katika
enep la Ilembo mjini hapa
Katika hutuba
yake ya uzinduzi huo Mwamlima
aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo kuwa
baraza hilo limeundwa na wajumbe
ishirini kutoka Serikalini na ishirini kutoka Sekta binafsi
ambapo mwenyekiti wa baraza hilo ni yeye Mkuu wa Wilaya
Alisema miongoni mwa malengo ya baraza hilo ni kuunganisha Serikali na taasisi
binafsi ili kuwaelimisha wananchi
wafanyabiashara watambue umuhimu wa kulipa kodi
kwani wafanyabiashara wasipo lipa
kodi nchi haiwezi kuendelea
Alifafanua kuwa kwa nchi changa mfanyabiashara ambae anakwepa kulipa kodi anajiona ni mjanja wakati kwa nchi zilizoendelea swala la
kulipa kodi ni lalazima na sio hiyari
Mwamlima alisema chombo hicho kinaowajibu wa kumuinua
mwananchi kwa kumsaidia
kwa kumuelimisha kibiashara na kumfanya aongeze kipato chake
Dc huyo aliwataka
wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha
wanaondoa migogoro yote ya
wafanyabiashara na kuwatafutia masako ya mazao yao ndani ya nchi na nje ya nchi yetu ya
Tanzania
Alisema
viongozi wa Wilaya ya Mpanda
wamekuwa wakitumia muda mwingi na gharama kubwa kushughulikia migogoro
hivyo baraza hilo litawapunguzia
mzigo huo viongozi wa Serikali na kuwafanya washughulikie zaidi shughuli za maendeleo badala ya migogoro
Kwa upande wake
afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Phosphor Nsuri
alieleza kuwa Wilaya ya Mpanda
imekuwa ikipokea wageni wengi wanaohamia
kwenye Wilaya hiyo kwa kasi kubwa kutokana na furusa mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo
Alizitaja baadhi
ya furusa hizo kuwa ni madini utalii
kilimo ufugaji uvuvi
katika mwambao mwa ziwa Tanganyika
Nae katibu
wa Baraza hilo Askofu Labani Ndimubenya
alisema kuwa Baraza hilo
litahakikisha linaimarisha mawasiliano ya ngazi ya Wilaya na ngazi ya Mkoa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment