Sunday, March 22, 2015

HII HATARI SANA: AKAMATWA NA VIUNGO VYA BINADAMU NA NYARA ZA SERIKALI‏


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa  Katavi  limemkamata na linamshikilia  Kulwa  Rajabu (35) Mkazi wa  Mtaa wa Kashaulili Wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za kumkamata na viungo  vinavyosadikiwa kuwa ni vya Binadamu na  nyara za Serikali    
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina  msaidizi  mwandamizi Dhahiri Kidavashari  mtuhumiwa huyo alikamatwa na viungo hivyo na nyara za  Serikali  hapo jana majira ya saa  tatu usiku   nyumbani kwake katika Mtaa wa Kashaulili mjini  hapa
 Alisema  mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia  taarifa ambazo zilikuwa zimelifikia jeshi la Polisi kutoka kwa Raia wema  ambao   walitowa taarifa kwa polisi kuwa mtuhumiwa ameifadhi viungo vya binadamu na  nyara  za Serikali ndani ya nyumba yake
 Alifafanua  baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi la polisi  walianza kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo  zilizokuwa zikimkabili  Kulwa Rajabu
Kamanda Kidavashari alieleza ndipo  hapo jana Polisi walipokwenda   nyumbani kwa mshitakiwa na walipofika nyumbani kwake walimfanyia upekuzi  huku wakiwa na viongozi wa Mtaa huo
 Alisema katika upekuzi huo Polisi  walifanikiwa kumkamata mshitakiwa  akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake  mifupa mitatu ,mshipa  mmoja  wa chini ya kinena unaodhaniwa  ni wa mtu mwanaume  na meno  mawili  viungo hivyo vinadhaniwa ni vya Binadamu
 Kidavashari alisema mbali ya mtuhumiwa  kukamatwa na viungo hivyo pia  mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake nyara za Serikali
 Alizitaja nyara alizokamatwa nazo mtuhumiwa  Kulwa Rajabu  kuwa ni  kipande cha ngozi  ya  Kalungu yeye  na singa mbili  za Tembo
Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani  ili akajibu mashitaka  mawili ya kupatikana na  viungo vinavyosadikiwa kuwa ni  vya Binadamu na kupatikana na nyara za Serikali

    

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment