Katavi
Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi kwa mwaka wa fedha wa 2015 na 2016 inatarajia kutumia na kukusanya Tsh 18,696,186,334.00 kutoka katika vyanzo vyanzo mbalimbali vya mapato
Hayo yalielezwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga wakati wa kikao cha sita cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini hapa
Akisema kati ya fedha hizo Ruzuku kutoka Serikali kuu itakuwa ni kiasi cha Tsh 16,507,934,362.00 ambapo mishahara itakuwa ni kiasi cha shilingi Biloni 9.3 Ruzuku ya matumizi ya kawaida itakuwa ni Tsh 1,167,392,200.00
Fidia ya mapato yaliyofutwa Tsh 233,328,500.00 na ruzuku ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ni kiasi cha Tsh 5,746,673,662.00
Lukanga alifafanua kuwa mapato ya ndani ambayo yatatokana na vyanzo vya mapato vilivyoko katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda wanatarajia kukusanya Tsh 1,147,482,972.00
Alisema miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2015 na 2016 imegawanywa katika sehemu mbili kuu ambazo ni miradi mipya na miradi viforo
Alieleza pamoja na kuandaa bajeti hiyo kwa kufuata vipaumbele vilivyopo maksio yameathirika kutokana na viwango vidogo vilivyowekwa na TAMISEMI na HAZINA hivyo hali hii imefanya mambo muhimu zaidi kutoweza kutengewa fedha au kutengewa fedha kidogo sana hivyo kutoleta matokeo stahili
Alisema kutokana na hari hiyo Halmashauri imewasilisha maombi maalumu nje ya ukomo wa Bajeti yenye jumla ya Tsh 2,988,500,000.00 hivyo kufanya jumla ya Tsh 21,684,686,334.00 zinazoombwa kwa mwaka wafedha ujao yaani Tsh 18,684,686,334.00 bajeti ya kawaida na Tsh 2,988,500,000.00 maombi maalumu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment