Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi ameigiza Kampuni ya Bytrade yenye makao yake makuu Mkoani Arusha inayowauzia wakulima mbegu za mahindi hapa nchini aina ya PIONEER Phb 3253 ameiagiza kampuni hiyo kumlipa fidia Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kumuuzia mbegu zisizo kuwa na ubora zilizoshindwa kuota baada ya kupandwa kwenye shamba lake lililoko Kijijini kwake Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi
Dr Msengi alitowa agizo hilo hapo jana kwenye shamba la Waziri Mkuu Pinda baada ya kulikagua shamba hilo lenye ekari sitini alipokuwa amefuatana na wataalamu mbalimbali wa kilimo wa wa Mkoa wa Katavi kufutia malalamiko mbali mbali yalikuwa yamepelekwa kwake na wakulima waliokuwa wamepanda mbegu za kampuni hiyo na kuwa zimeshindwa kuota likiwemo shamba hilo la Pinda
Awali Afisa kilimo wa Mkoa wa Katavi Shanal Nyoni alimweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa shamba hilo la Pinda lina ukumbwa wa ekari sitini ambazo zimelimwa na kupandwa mahindi kati ya hizo ekari 29 zilipandwa mbegu za mahindi za kampuni ya Bytrade aina ya Pioneer Phb 3253
Nyoni alieleza kati ya ekari hizo ekari tisa zimeshindwa kuota kabisa kutokana na mbegu hizo kutokuwa na ubora licha ya eneo hilo kupandwa kwa usimamizi wa karibu wa wataalamu wa kilimo ambao hulitumia shamba hilo kama shamba darasa kwa wananchi wa Kata ya Kibaoni
Alieleza shamba hilo pia limepandwa mbegu za mahindi za kampuni ya Monsanto aina ya Dk c 9089 ambao zimeota zenye bila shida yoyote ile tofauti na mbegu hizo
Alisema tatizo la mbugu za kampuni hiyo kupandwa na kushindwa kuota limetokea pia kwa wakulima wengine wakata za Kibaoni Usevya ,Mamba na Itenka katika Wilaya ya Mlele Mkoani hapa
Akitowa agizo hilo Dr Msengi alisema mbegu zilizotumika kupandwa kwenye shamba hazikuwa nzuri na wala hazikiwa na ubora unasitahili
Alisema lengo la Serikali ni kumsaidia mkulima ili aweze kuongeza uzalishaji na sio kumfanya mkulima avunjike moyo kwenye jitihada zake za kilimo
Alifafanua kuwa Serikali haitakubali kuona nguvu za wakulima zikiwa zinapotea bure kwa faida ya watu wachache wanaotaka kujinifaisha kwa kuwauzia mbegu mbevu wakulima na Serikali ya Mkoa wa Katavi itahakikisha inayathibiti makampuni yote ambayo yanataka kupoteza bure nguvu za wakulima
Alisema Mkoa wa Katavi hautasita kuyafutia leseni makampuni yatakayo bainika yanasambaza kwa wakulima pembejeo za kilimo ambazo hazina ubora
Dr Msengi aliziagiza Halmashauri zote nne za Mkoa wa Katavi kufanya tathimini ya mashamba yote ambayo yalipandwa mbegu za kampuni hiyo na zimeshindwa kuota na wakulima hao walipwe fidia na kampuni hiyo
Alisema gharama wanayositahili kulipwa ni wakulima wote na sio Pinda Peke yake na wataalamu hao wazingatie pia na muda waliotumia wakulima pamoja na nguvu zao
Alisema kwa hilo yeye kama Mkuu wa Mkoa hana wasilaha hata kidogo na uamuzi wake huo hivyo wataalamu wa Kilimo wahakikishe baada ya siku saba wawe wamempa utekelezaji wa maagizo hayo
Kwa upande wake meneja wa mbugu wa kampuni hiyo ya Bytrade Rajab Athuma alimweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa tayari kampuni hiyo imeanza kupanda upya mbegu nyingine kwenye shamba hilo la Pinda na tayari wamepanda ekari nne na bado wanaendelea
Alisema hata hivyo anawasiwasi na utaalamu uliotumika wakati wa kupanda shamba hilo kuwa inawezekana kulikuwa na kasoro
Kauli hiyo ilipingwa vikali na Mkuu wa Mkoa pamoja na afisa kilimo kwa kile walichomweleza kuwa wakati wa upandaji wa mbegu hizo nawao walishiriki kupanda
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO KATIKA MIAKA 5 IJAYO? JAZA FOMU FUPI HAPA
No comments:
Post a Comment