Na Walter Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewakamata na linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuwakamata na meno ya Tembo vipande 22 yenye uzito wa kilogramu 46 yenye thamani ya shilingi milioni 157,500,000 sawa na Tembo saba waliouwawa wakati wakiwa wanataka kuyasafirisha kwenye basi kutoka Mpanda kuyapeleka Mkoa wa Kigoma
Kaimu Kamanda wa wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Rashid Mohamed aliwataja watuhumiwa hao waliokamatwa kuwa ni Justine Baluti (Zolros)(39) Mkazi wa Kijiji cha Ivungwe makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na Bobifaphace Hoza (40) Mkai wa Kalele Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma
Alisema watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa hapo jana majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika eneo la stendi ya mabasi ya Mpanda iliyoko katika mtaa wa Mji wa Zamani mjini Mpanda
Siku hiyo ya tukio majira hayo ya saa kumi na mbili asubuhi Askari Polisi walikuwa dolia kwenye eneo la stendi ya mabasi ya Mpanda yaendao Mikoani walimtilia shaka mtuhumiwa Justine Baluti aliyekuwa anapakia mizigo yake kwenye basi la Kampuni ya Adventure lenye Namba za usajiri T.992 BUT aina ya Nissani lililokuwa likielekea Mkoani Kigoma
Kaimu Kamanda Rashid Mohamed alieleza baada ya polisi kumtilia mashaka mtuhumiwa huyo na yeye alipowaona polisi kwenye eneo hilo alitaka kutoroka kwenye eneo hilo hata hivyo polisi walifanikiwa kumweka chini ya ulinzi
Polisi baada ya kupekua mizigo ya mtuhumiwa Justine walimkuta akiwa na meno ya Tembo vipande 15 yenye uzito wa kilogramu 33 vyenye thamani ya Tshilingi milioni 90 sawa na Tembo wanne waliouwawa yakiwa ameyahifadhi ndani ya mabegi makubwa mawili
Alisema baada ya Justine kupekuliwa na kukutwa na meno hayo ya Tembo mtu mwingine ambae inaonesha alikuwa na mtuhumiwa alitupa beji lake la rangi ya ugoro na kisha kutokomea kusiko julikana
Polisi waliweza kulikamata Basi hilo la Kampuni ya Adventure na kulipeleka hadi kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya upekuzi zaidi
Kaimu Kamanda Rashid alisema baada ya polisi kufanya ukaguzi wa kina kwenye basi hilo walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Bonifaphace Hoza akiwa na beji moja alilokuwa amelihifadhi chini chini ya siti Namba K.3 Lililokuwa ndani yake na vipande saba vya meno ya Tembo yenye uzito wa kilogramu 13 yenye thamani ya Tsh milioni 67,500,000 ambayo ni sawa na tembo watatu waliouwawa
Alisema watuhumiwa hao wawili wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili wajibu tuhuma zinazowakabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment