Sehemu ya barabara ya kutua na kurukia ndege katika
Uwanja wa Ndege wa Mpanda.
Sehemu ya Uwanja wa ndege wa
Mpanda ikiwa imekamilika kwa kiwango cha lami.
Meneja wa Uwanja wa ndege wa
Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kushoto) akimuonesha kitu Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia). Wanaoshuhudia ni wajumbe wa timu hiyo
Meneja wa Uwanja wa ndege wa
Mpanda, Mkoani Katavi Bw. Seneti Lyatuu (Kulia) akifafanua jambo kwa Kiongozi
wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto). Anayewasikiliza ni Kaimu Mkurugenzi wa
Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Abdallah (Katikati).
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
(Kushoto) akizungumza na Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mpanda, Mkoani Katavi Bw.
Seneti Lyatuu (Kulia). Anayefuatilia mazungumzo ni Bw. Omary Abdallah ambaye Kaimu
Mkurugenzi wa Mipango na Ufuatiliaji (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango).
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Mpanda kujionea shughuli mbalimbali za maendeleo uwanjani hapo.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelekezo ya
uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda kutoka kwa Meneja wa uwanja huo, Bw. Seneti
Lyatuu (Kushoto).
---
Na Saidi Mkabakuli, Mpanda
Kufuatia kukamilika kwa ukarabati na upanuzi
wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, mkoani Katavi, Serikali imewaasa watumiaji wa
uwanja huo kutunza miundombino ya uwanja huo ili kuweza kuhudumia wakazi na
wageni wapitao uwanjani hapo kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya
miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa
Mpanda, mkoani Katavi.
Bibi
Mwanri alisema kuwa serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege imekamilisha kazi
ya kuufanya uwanja huo uwe wa kiwango kizuri tayari kwa kutumika kwa ndege za
binafsi na biashara, hivyo uongozi wa uwanja huo hawana budi ya kuhakikisha
miundombinu ya uwanja huo inatunzwa ipasavyo.
“Kama munavyofahamu Serikali imekuwa ikiwekeza sana katika uendelezaji wa
miundombinu ya usafiri nchini hasa kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri
wa anga ili kuongeza ufanisi na kuendelea na kazi ya ujenzi na ukarabati wa
viwanja vya ndege katika maeneo ya kimkakati, hivyo kuna haja ya kuunga mkono jitihada
hizi za Serikali,” aliasa Bibi Mwanri.
Akitoa taarifa ya uendelezaji uwanja huo kwa msafara wa timu ya ukaguzi, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Bw Seneti
Lyatuu alisema uwanja huo umeboreshwa na hivyo, unaweza kutumika kutua na
kuruka ndege za kiwango cha kati na hata zile ndege kubwa zinaweza kutua kwa
dharura.
“Uwanja huu umekarabatiwa na barabara ya
kuruka na kutua ndege imerefushwa kwa kiwango cha lami kutoka urefu wa mita
1,500 na upana wa mita 30 hadi kufikia urefu wa mita 1,820 na upana wa mita 30,”
alisema Bw. Lyatuu.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, kukamilika kwa
uwanja huo kumevutia idadi ya abiria wanaoutumia uwanja huo kutoka abiria 285
mwaka 2009 hadi 2,390 mwaka 2013/14.
Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza,
hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji (bandari,
reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji) na
TEHAMA.
Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka
Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo
kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka
misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi.
Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa
mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na
kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya
maendeleo kitaifa.
Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa
nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment