Na Walter Mguluchuma, Katavi yetu
MTOTO mwenye
umri wa mwaka mmoja na miezi miwili ,
Regina Geofrey ameuawa kikatili kwa kunyongwa
na baba yake mzazi Geofrey Kilngwa ‘Simbaiwe” (27) kwa kuwa
alizaliwa akiwa ameatanguliza makalio
yake .
Baba wa binti huyo
ambaye pia mganga wa
kienyeji anayeishi kitongoji cha Mwikang’ombe,
kijijicha cha Katuma ,wilayani Mpanda alitenda
unyama huo kwa mdai kuwa mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio yake ni mkosi na nuksi kubwa katika shughuli zake hizo za uganga wa kienyeji .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari akizungumza leo na waandishi wa habari mjini hapa amedai kuwa
mzazi huyo aliyetenda uhalifu huo Julai 20 mwaka huu
ambapo alikamatwa na jeshi la Polisi Agosti 26, mwaka huu..
Inadaiwa siku hiyo ya
tuki mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake huyoalimzika
kwa siri katika kibanda
chake anachofanyia shughuli zake za uganga wa kienyeji .
Akisimulia mkasa huo
Kamanda Kidavashari alidai kuwa mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa
ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi
mmoja .
“Ndipo baba
mzazi wa
binti huyo alipoalazimika kuanza kumuuguza kwa siri
pasipo mama yake mzazi
kufahamu kwani alimdanganya kuwa mtoto
wao huyo amepelekwa kutibiwa
na babu yake huko mkoani Mwanza “
alieleza Kidavashari .
Inadaiwa kuwa kibanda
ambacho mtuhumiwa alikuwa akifanyia
shughuli zake za uganga
kilikuwa mbali na makazi yake hivyo
ilikuwa rahisi kumficha mtoto
wake huyo kwa zaidi ya mwezi mzima akimtibu
bila mama mzazi wa mtoto huyo
kufahamu .
Kwa mujibu wa kamanda Kidavashari ,wakazi wa kitongoji cha Mwikan’gombe wakiongozwa na Mwenyekiti wao walimtilia shaka mtuhumiwa
kutokana na tetesi
zilizozagaa eneo hilo kuwa mtoto Regina alikuwa ameuawa na baba yake
mzazi na kuzikwa kwa siri .
Inadaiwa wakazi hao
na mwenyekiti wao waliamua kufika
nyumbani kwa mtuhumiwa na kuhoji
alipo binti yake Regina ambapo alipinga
vikali lakini alipopekuliwa katika kibandani kwake walibaini kuweko kwa tuta dogo
lililkuwa limechimbwa siku za
karibuni .
Kidavashari aliongeza
kuwa wakazi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao
waliamua kufukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto
huyo kisha wakaitaarifu polisi .
Mama ya marehemu aitwae Maria Exavery (22) alidai kuwa
hakuhusishwa wala kupewa taarifa kwamba binti yake huyo amekufa “Mie nilikuwa nafahamu kuwa
Regina yuko kwa
babu yake , Mwanza akitibiwa “
alieleza .
Nae Regina Kaboni (40) mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na mtuhumiwa anadai
kuwa alishirikishwakatika maziko ya binti huyo “hata hivyo nilishtushwa sana kwa kitendo
cha mtuhumiwa kumzika mwanae bila ya kumshirikisha mkewe , nilipomuuliza
mtuhumiwa alidai kuwa kwa mila ya
kwao mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio yake mama mzazi wa mtoto
ni mwiko kushirikishwa katika maziko ya mtoto huyo ‘ anadai
Kwa mujibu wa Kidavashari
watu wanne wakiwemo wazazi
wa marehemu wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi
ambapo watafikishwa mahakamani mara
tu baada ya upelelezi wa awa;li kukamilika
..
Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi hilo
ni pamoja na Regina Kaboni na
Msolwa Jacob (29) mkazi wa kitongoji cha
Mwikanga’ombe .
No comments:
Post a Comment