Wednesday, September 24, 2014

ACHINJA MKEWE WATOTO WAKISHUHUDIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
POLISI mkoani Katavi wanamsaka mkazi wa kijiji cha Urwila wilayani Mlele, Mohamedi Katyukuru (49) kwa kumuua mkewe kwa kumchinja.
Inadaiwa mwanaume huyo alifanya mauaji hayo Septemba 14 mwaka huu wakati watoto wao wawili, wenye umri wa kati ya miaka 11 na 14, wakishuhudia.
Inadaiwa baada ya mauaji hayo, alitoroka pamoja na watoto hao na kujificha kusikojulikana.
Alifunga mlango kwa nje na kufanya majirani wachukulie kwamba ametoka kwenda kwenye shughuli zake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alimtaja aliyeuawa kuwa ni Bernadeta Mwetel (38), ambaye mumewe alikuwa akimtuhumu kuwa na uhusiano na mwanamume mwingine.
Chanzo:Habari Leo

No comments:

Post a Comment