Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na
Walter Mguluchuma
Jumla ya Ng’ombe kumi
na Moja na mbuzi wanne
wameuwa na kuliwa na mnyama simba
katika matukio matatutofauti yaliyotokea
katika Tarafa ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi baada ya simba kuvamia katika
vijiji vitatu
Kwa mujibu wa
Diwani wa Kata ya Mtapenda Elieza Fyula
tukio la kwanza lilitokea hapo
Mei 28 majira ya usiku katika Kijiji
cha Kabatini
Katika tukio
hilo Simba wa
walivamia kwenye kijiji hicho na kuuwa na kula Ng’ombe
watatu na mbuzi watano
ambao walikuwa wako ndani ya zizi
la kufugia mifugo
Alisema siku
iliyofuata ya tarehe 29 meimajira ya usiku simba hao
walivamia katika Kitongoji cha Kambike
kilichoko katika Kijiji cha Isinde na
kuwauwa Ng’ombe watano mali ya mfugaji wa kitongoji hicho aitwaye Dirisha
na kisha waliwala ng’ombe hao
DiwaniFyula alieleza
baada ya tukio hilo viongozi wa kitongoji walitoa taarifa kwa viongozi wa kata
ambao waliwasiliana na Idara ya Wanyama
Poli ambao waliwasili kijijini hapo na kuwaswaga simba hao wapatao watano
Alisema siku
iliyofuata simba hao walivamia tena kwenye kijiiji cha mkumbi na kisha waliuwa Ng’ombe wawili na
kuwala
Na Blogs za mikoa

No comments:
Post a Comment