Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za
kumuuwa Bodaboda mmoja aitwaye
Frenk Joseph (25)mkazi wa mtaa wa
Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinjashigo na kisha kumpola pikipiki yake
aina ya SANLG yenye namba za usajiri
T 704 CDQ
Kamanda wa jeshi
la Polisi wa Mkoa wa KataviKamishina msaidizi
mwandamizi Dhahiri Kidavashari
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Charles Kidaha(29),Madia Mtema
(40) na Buyenza Jendesha (40) wote
wakazi wa Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda
Kidavashari alisema
watuhumiwa hao walimuuwa bodaboda
huyo hapo Aprili
26 mwaka huu majira ya saa saa kumi na moja jioni huko katika eneo la
Kijiji cha Mpembe Tarafa ya Mwese
Wilayani Mpanda
Siku hiyo ya
tukio marehemu Samwel alikuwa kwenye kijiwe chake cha Bodaboda kilichoko kwenye
hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa na pikipiki yake aina ya Sunlg yenye
Namba za usajiri T704CDQ a
Alisema wakati akiwa kwenye
kituo hicho cha Bodaboda
alitokea mtu asiye fahamika na kumkodisha marehemu ambapo waliondoka
nae huku marehemu akiwa aja waagabodaboda na kuwafahamisha mahari
alikokuwa wakielekea
na mteja wake huyo
Alifafanua kuwa
ndipo siku iliyofuata ya tarehe 27 Aprili
mwili wa marehemu bodaboda huyo
ulipoonekana ukiwa
umetelekezwa porini katika kijiji
cha Mpembe huku akiwa amechinjwa na kitu chenye ncha
kali na pikipiki yake haikuonekana katika
eneo hilo
Kamanda
Kidavashari alieleza kuwa baada ya
tukio la mauwaji hayo polisi
waliendelea kufutilia tukio hilo kwa kushirikiana na raia wema
na ndipo hapo mei 22 majira
ya saa kumi na moja jioni huko katika kijiji cha Kasekese
Kata ya Simbwesa Wilaya ya Mpanda raia wema walitowa taarifa kwa jeshi la
polisi kuwa wanamashaka na watuhumiwa hao kwani waliwasili kijijni
hapo wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki moja
Alisema baada ya
taarifa hizo jeshi la polisi liliweza kufanikiwa kufika kijijini hapo
mara tuu baada ya muda mfupi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote
watatu wakiwa na pikipiki hiyo ya
marehemu Samweli waliompola baada ya
kumuuwa
Katika maojiano
ya awali baini ya jeshi la polisi na
watuhumiwa hao watatu imeonyesha kuwa
watuhumiwa hao ndio
waliohusika na mauwaji ya bodaboda huyo
Kamanda
Kidavashari ameleza watuhumiwa hao
wote watatu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamiliki
No comments:
Post a Comment