Tuesday, May 27, 2014

JELA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUMBAKA SHEMEJI YAKE (13)

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama  ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  imemuhukumu Philipo Emanuel (35)Mkazi wa  Mtaa wa Mpanda Hotel  mjini Mpanda  kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kumbaka shemeji yake   msichana (13) mdogo wa mke wake  mdogo
Hukumu  hiyo imetolewa  hapo juzi na  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama  kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pambe  zote mbili za upande wa mashitaka na utetezi
Mshitakiwa  alidaiwa kutenda kosa hilo la kumbaka mdgo wa mke wake hapo  Septemba  24 mwaka jana  majira ya saa moja na nusu usiku huko katika  eneo la mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda
Awali katika kesi hiyo  mwendesha mashitaka  Godfrey  Ruzabila aliiambia mahakama kuwa siku hiyo ya tukio msichana huyo aliyebakwa  alikuwa ametumwa  dukani na dada yake   kwenda  kununua mafuta ya kupikia mlo wa jioni
Alieleza wakati  msichana huyo akiwa anaelekea  dukani ndipo   alikutana na mshitakiwa  ambae alimwita  msichana   huyo  na kisha   alimwomba  amsindikize dukani alikokuwa anakwenda  kununua mafuta ya kula aliyokuwa   ametumwa na dada yake
Mwendesha mashitaka alidai  baada ya kuwa wamefika dukani  msichana huyo alinunua mafuta  na kisha  mshitakiwa alimweleza shemeji yake kuwa anataka kumnunulia zawadi  dukani hapo   hivyo achague  kitu gani anachokihitaji ndipo msichana huyo alipomweleza shemeji yake kuwa yeye anahitaji Biscut na Pipibomu
Mshitakiwa baada ya kumnunulia shemeji yake zawadi hizo alimtaka amsindikize  alikokuwa  akienda   ombi ambalo  msichana huyo alilikubali  kwani   hakuwa na mashaka yoyote ya kusindikizwa  na shemeji yake
Mwendesha mashitaka alieleza wakati wakiwa  njiani mshitakiwa Philipo  Emanuel alimwingiza msichana huyo kwenye pagara  na kisha alipiga ngwala  na kuanza kumbaka  huku msichana akijaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini alishindwa kutokana na mshitakiwa muda wote kuwa  amembana mdomo
Alieleza  baada ya kuwa amemaliza kumfanyia unyama huo alipatia mtoto huyo shilingi elfu  moja kama malipo yake  na  shilingi elfu tano alimpatia  iliamfikishie dada yake  na alimkaza asimwombie  mtu yoyote yule kuwa amefanyiwa  kitendo hicho na mshitakiwa
Ruzabila alisema  baada ya msichana kufika nyumbani kwao dada yake alimuuliza  kwanini amechelewa kurudi  ndipo binti huyo alimweleza dada yake njisi ambavyo shemeji yake alivyomfanyia hari ambayo  ilmshitua dada yake na kumfanyaachukue uamuzi   wa kumvua nguo na kumkagua  katika sehemu zake za siri  na kukuta anatokwa na damu hari ambayo ilimfanya ashituke   na kupelekea kuamua kutoa taarifa kwa wapangaji wenzake 
Alieleza dada wa binti na  majirani walimtaka msichana huyo awapeleke kwenye eneo alilofanyiwa unyama huo na walipofika kwenye eneo la tukio waliingia ndani ya pagala na kukuta Paketi ya Biscuti aliyokuwa amenunuliwa na shemeji yake  huku pembeni kukiwa na mafuta ya kula yaliyomwagika na ndipo walipo amua kwenda kituo cha polisi cha mpanda na kutoa taarifa
Katika kesi hiyo  upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi wanne  akiwemo Daktari ambae alithibitishakuwa msichana huyo alifanyiwa kitendo cha ubakwaji   baada ya  kufanyiwa uchunguzi wa kidakitari  na  kukutwa na mbegu za kiume na upande wa utetezi ulikuwa na mashahidi wanne
Hakimu mkazi  Chiganga Ntengwa  baada ya kusikiliza mwenendo mzima wa kesi  aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa Philipo Emanuel  amepatikana na hatia  ya kosa la kifungu namba 130 (1) (2) hivyo mahakama  inampa nafasi mshitakiwa kabla ya kutolea kwa adhabu kama anayo sababu ya msingi ya kuishawishi mahakama impunguzie adhabu
Katika utetezi wake mshitaki aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anafamilia ya wake  wawili ambao wanamtegemea  pamoja na watoto  ombi ambalo lilipingwa na mwendesha mashitaka
Baada ya utetezi huo hakimu  Chiganga alisoma hukumu kwa kueleza kuwa  kutokana na mshitakiwa Emanuel Philipo kupatikana na kosa hilo mahakama imemuhukumu kwenda jela kutumikia  kifungo cha miaka 30 jela  kuanzia mei   26  mwaka huu

No comments:

Post a Comment