Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima amekea tabia ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda kukimbilia huhudhuria kwa wingi kwenye vikao wanavyolipwa posho na kuvikimbia kuhudhuria vikao ambavyo hawalipwi posho
Mwamlima alitowa kauli hiyo hapo juzi kwenye mkutano wa wadau wa uzinduzi wa mchakato wa uanzishwaji wa mfuko wa Afya ya jamii wa utoaji huduma ya matibabu kwa kadi TIKA uliofanyika kwenye ukumbi wa idara ya maji
Alisema wakuu wa Idara zilizopo kwenye Halmashauri ya Mji wa Mpanda wamekuwa na tabia ya kutohudhuria vikao vinavyokuwa vimeitishwa ambavyo wanajua hawata lipwa posho
Alieleza kushangazwa na idadi kubwa ya wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye kikao hicho tofauti na wanavyo hudhuria kwenye vikao vingine
Alifafanua kuwa wakuu wa Idara wamehudhuria kwa wingi kwenye kikao hicho kwa kuwa wamejua kikao hicho kinamalipo ya posho ya kikao
Alisema babia hiyo ya kukimbilia kwenye vikao vyenye posho ni vizuri wakaiacha mara moja kwani sio tabia nzuri kwa viongozi kukimbilia vikao vyenye malipo na kuvikimbia vikao ambavyo havina malipo
Hivi karibuni Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpanda alikuwa na ziara ya kutembelea kata mbalimbali za Halmashauri ya Mji wa Mpanda kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kufanya mikutano ya hadhara akiwa anatakiwa kuwa na wakuu mbalimbali wa idara lakini walikuwa wanajitokeza wakuu wa idara wachache sana kwenye ziara hiyo
Hari hiyo ya kutojitokeza kwa wakuu wa idara wachache kwenye ziara hiyo ambayo ilikuwa haina malipo yoyote ilisababisha Mkuu huyo wa Wilaya akasirishwe na kitendo hicho ambapo kwenye ziara yake ya mwisho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Kata ya Makanyagio alitaka kulazimika kutaka kuwaweka mahabusu wakuu wa idara wote ambao hawakuhudhuria ziara siku hiyo
No comments:
Post a Comment