Sunday, April 20, 2014

BODABODA AJIZUSHIA KIFO BAADA YA KUNYANG'ANYWA PIKIPIKI NA BABA YAKE KWA KUMUHOFIA KUPATA AJALI WAKATI WA SIKUKUU YA PASAKA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma 
Mpanda  Katavi 
Katiika  hari  isiyoyakawaida Mwendesha Pikiki Bodaboda  Mohamed Kalyalya   24  Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Madukani Wilayani hapa amejizushia  kifo  baada ya kukasirishwa  na kitendo cha  baba yake  kumnyang’anya pikipiki  kwa kumuhofia  kupata ajali katika  sikukuu ya Pasaka 
Tukoio hilo la Bodaboda kujizushia kuwa amefariki  Dunia  lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na moja jioni ikiwa ni siku moja baada ya baba yake mzazi  kumnyanga’anya pikipiki  ambayo alikuwa amemkabidhi aitumie  kwa shughuli  za Bodaboda  kitendo ambacho kilimkasirisha kijana huyo 
Siku hiyo ya tukio Mohamed  akiwa  na rafiki yake  aitwaye Kaduga Antoni  ambae wanafanyanae  shughuli ya Bodaboda katika eneo la  Bar  ya White Club  alimshawishi rafiki yake huyo  awapigie simu  wazazi wake kwa kutumia simu yake ya mkononi  ili awafahamishe kuwa   Mohamed amefariki Dunia baada ya kujiuwa kwa kunywa sumu 
Bodaboda huyo mwenzake baada ya kushawishiwa hivo  alipiga simu kwa wazazi wake na Mohamed  na kuwapataarifa za kifo cha mtoto wao  alifariki Dunia  kwa kunywa sumu akiwa katika maeneo ya vichaka vya Shanwe mjini hapa   na taarifa hiyo aliwapigia Bodaboda wenzake wanaofanya shughuli  kwenye kituo cha Bar ya White Club
Wazazi wa Bodaboda  walipopata taarifa hizo  walianza  kulia na majirani  walifika kwenye  eneo  hilo la nyumbani kwao na Bodaboda kwa ajiri ya kuomboleza  msiba kwa jirani yao  na walianza shughuli za  kuuweka mji huo katika mazingira ya usafi kwa ajiri ya kuweka msiba 
Wakati harakati hizo za kuweka msiba zikiwa  zinaendelea  Bodaboda wenzake waliamua  kwenda kumtafuta mwenzao kwenye eneo ambalo alidaiwa  kuwa amefia  kwa kujiuwa kwa kunywa sumu 
Bodaboda hao walifika katika eneo hilo ambalowalikuwa wameambiwa  amefia mwenzao  hata hivyo  walifanya jiitihada za kumtafuta kichakani na hawakuweza  kufanikiwa kumwona  kwenye  eneo hilo 
Jitihada za kumtafuta ziliendelea  ndipo  wakati Bodaboda walifika kwenye eneo la mtaa wa Kigamboni  walimwona Mohamed akiwa anatembea barabarani na walipomsemesha alitaka kuwakimbia na kisha walimsihi  awaeleze sababu iliyomfanya ajizushie kifo 
Katika maelezo yake alieleza kuwa  rafiki  Kaduga Anton ndiye aliye chukua simu yake    ya mkononi na kuwasambazia wazazi wake    na Bodaboda taarifa za kifo chake hicho 
Kwa upande wake Kaduga aliwaeleza kuwa Mohamed alimpatia simu yake na kumweleza awapigie simu wazazi wake kuwa amekunywa sumu na amefariki Dunia  na aliamua kufanya hivyo kwa kuwa baba yake siku moja kabla ya tukio hilo alimyang’anya pikipiki  kwa kile alimweleza kuwa     na wasimasi na mtoto wake kupata ajali wakati wa sikukuu ya Pasaka kutokana na tabia yake ya ulevi

No comments:

Post a Comment