Thursday, March 27, 2014

MAJENGO YA WANAFUNZI YA SHULE YA WASICHANA YASHINDWA KUTUMIKA KUTOKANA NA UKOSEFU WA WANAFUNZI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baadhi ya Majengo ya madarasa  yaliyojengwa katika  Shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda  hayajawahi kutumika    tangia yalipopo jengwa  mwaka 2010 na yameanza kuchakaa  kutokana na Wizara ya Elimu  mafunzo na ufundi  kushindwa kupeleka wanafunzi shuleni hapo
Hayo yalielezwa hapo juzu na Mkuu wa Shule hiyo  Nyabise Sabasi  mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima alipotembelea shuleni hapo kwa lengo lakufanya  ziara ya shule hiyo ya kukagua ujenzi wa ukarabati wa shule hiyo
Alisema shule hiyo ya wanafunzi i wasichana ya Kidato  cha tano na  cha sita ambayo inajumla ya majengo ya vyumba vya madarasa 30  ilifunguliwa mwaka wa 1986 na inakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo  kuwa ni uchache wa  wanafunzi wanaopelekwa shuleni hapo  ambapo shule hiyo inauwezo wa  kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita wanafunzi 840 wakati waliopo ni 253  hari ambayo imesababisha  baadhi ya majengo ya madarasa  yaliojengwa toka mwaka 2010  kushindwa kutumika hadi sas
Changamoto nyingine ni  majengo mengi ya  mabweni  licha kuwa na vitanda yako wazi kutokana na kukosa wanafunzi wa kulala kwenye mabweni hayo
Kwa upande wake mwanafunzi wa shule hiyo Magdalena  Yanga  alimweleza Mkuu wa Wilaya  kuwa  shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa  shule hiyo kutokuwa na gari lolote la usafiri  pamoja na  kutokuwa na zahanati  hari ambayo inawazimu wanafunzi kuacha masomo  na kuwasindikiza  hospitali pindi wanapo kuwa wameugua
Nae mkuu wa Wilaya ya Paza Mwamlima aliwataka wanafunzi wa  shule hiyo wahakikishe wanaongeza bidii ya  kusoma ili watakapo faulu vizuri  waje kuisaidia Serikali hapo baadaye na kuhusu mganga Serikal Imepangia  kazi watumishi mbalimbali wa kada ya afya hivyo watakapo lipoti mwezi ujao  watapewa mganga hivyo ni vizuri uongozi wa shule ukaandaa nyumba ya kuishi shuleni hapo kwa Daktari 
 Alisema mwaka jana shule hiyo ilikuwa ni ya 69  Kitaifa  kwa matokeo ya kidato cha sita kwa hari hiyo ni vizuri mwaka huu  shule hiyo ikashika nafasi za juu zaidi  hata vyo wanafunzi hao walihaidi mbele ya mkuu huyo wa Wilaya kuwa mwaka huu watashika nafasi tatu za juu za ufaulu Kitaifa

No comments:

Post a Comment