Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma, Mpanda - Katavi
NDUGU
wawili wa kiume wa familia moja ambao ni wakazi wa Kitongoji cha
Milumba , Kata ya Kibaoni ,wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi
wanadaiwa kumuua kikatili, K itungulu Luhende (65) kwa kumchinja na
kuutelekeza mwili wake porini.
Taarifa
kutoka katika eneo la tukio hilo pia kuthibitishwa na polisi
zinadai wa kuwa chanzo cha ndugu hao wawili kufanya unyama huo
inadaiwa ni wivu waliokuwa wakimwonea Luhende ambaye anadaiwa kuwa
hawala wa mama yao , kwa kufanya na mama yao mapenzi mara kwa mara
tena bila kificho .
Inadaiwa
mama yao aitwae Sai Mponjie (65) ni mjane ambapo kwa muda mrefu
sasa amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yao .
Akithibitisha
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari aliwataja
wanandugu hao ni pamoja na Luhende Kashila (16) na kakae Nyengu
Kashila (19) ambao wanatuhumiwa kumuua kikatili ‘hawala’ ya mama
yao .
Akisimulia
mkasa huo , Kidavashari alidai kuwa Februari , 22 , mwaka huu saa
mbili asubuhi , Luhende ambae pia ni mkazi wa Kitongoji hicho cha
Milumba alimwaga mkewe ambaye jina lake halikuweza kufahamiaka mara
moja kuwa anaenda kijijini Kirida ambako pia ana mji mwingine .
“Hata
hivyo inadaiwa marehemu badala ya kwenda kijijini Kirida mwenye
mji wake mwingine alipitia nyumbani kwa rafiki yake katika
kitongoji hicho cha Milumba , aitwae Milembe Katembeni ambako
aliiacha pikipiki yake yenye aitwae Sai “ alidai Kamanda
Kidavashari.
Indaiwa
kuwa marehemu hakuweza kuonekana tena hadharani hadi mwili wake
uligundulika ukiwa umetekelezwa katika eneo la milima ya
kitongoji hicho cha Milumba ukiwa tayari umeshaharibika kufuatia
msako mkali uliofanywa na askari Polisi na askari wa jadi
‘sungusungu’huku pembeni ya mwili huo wa marehemu iliokotwa leseni
yake ya udereva Daraja A.
“Baada
ya marehemu kutorejea kuchukua pikipiki yake rafiki yake aliingia
wasiwasi baada ya wiki kupita bila Luhende kuonekana na kuchukua
mali yake hivyo aliamua kutoa taarifa kwa Mtemi wa Sungusungu
katika Kitongoji hicho kisha akatoa taarifa katika Kituo kidogo
cha Polisi cha Kibaoni ndipo msako mkali ulipoaanza “anadai Kamanda .
Kwa
mujibu wa Kidavashari chanzo cha mauaji hao ni wivu wa watoto hao
baada ya kuona marehemu akifanya mapenzi na mama yao mara kwa
mara kitendo kinachodaiwa kuwakera sana watoto hao .
Anaongeza
kuwa tayari mama ya watoto hao Sai Mponje (65) na mwanae aitwae
Luhende Kashele (16) wanashilikiwa kwa mahojiano huku polisi
ikimsaka mtoto mwingine aitwae Nyengu Kashele (19) ambaye
alitoroka mara baada ya kufanyika kwa mauaji hayo na kujificha
kusikojulikana .
No comments:
Post a Comment