Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Kalenga
Mashaka 52 Mkazi
wa Kijiji cha Kusi makazi ya
wakimbizi yamishamo
Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kupigwa
na kitu kizito kichwani
na watu wasiojulikana
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina Maidizi Mwandamizi Dhahiri
Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo
juzi majira ya saa mbili asubuhi kijijini
hapo
Alisema katika
uhai wake marehemu aliwahi kufikishwa
katika uhai wake marehemu aliwahi kufikishwa katika mahakama ya
mwanzo ya Mishamo kwa kutuhumiwa kutishia kuuwa kwa maneno ambapo
alikuwa akiwatishia watu kuwauwa
kwa njia ya ushirikina
Kamanda
Kidavashari alifafanua kuwa kitendo hicho cha kuwatishia wakazi wa kijiji hicho
kwa njia ya ushirikina kilijenga chuki baina ya marehemu na wanakijiji
hicho
Alifafanua
kuwa kwa
mujibu wa uchunguzi wa awali chanzo
hicho kutishia kuwauwa kwa
ushirikina wanakijiji wenzake ndicho
kilichosababisha kutokea kwa mauwaji ya mtu hoyo
Alisema kuwa wanakijiji
hicho cha Kusi walikuwa
wamechoshwa na vitendo hivyo vya
kutishiwa kuondolewa uhai wao kwa njia ya ushirikina alivyokuwa akivifanya
marehemu Kalenga
Kidavashari alieleza
kabla ya tukio la marehemu
kufikishwa kwenye mahakama ya
mwanzo ya Mishamo wanakijiji hicho waliwahi kujichukulia sheria
mkononi kwa kuichoma moto nyumba
ya marehemu kwa lengo la kumfukuza kijini hapo
Polesi
wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
ili kuwabaini watu au mtu aliyehusika na mauwaji hayo ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
No comments:
Post a Comment