Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Shoma Salumu (78) Mkazi wa Kata ya Kakese Mkwajuni
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekutwa akiwa ameuwawa kwenye chumba
chake kwa kukatwa mapanga
sehamu za kichwani na juu ya sikio na watu wasiojulikana
Kwa mujibu wa Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Katavi
Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji hayo lilitokea hapo Desemba 29 majira ya
saa mbili na nusu asubuhi kijijini
hapo nyumbani kwa motto wa marehemu aitwaye Lameck Mboka
Alisema siku moja kabla ya tukio hilo hapo
majira ya saa saba mchana marehemu
akiwa katika shughuli
zake za kila siku za
kufinyanga vyungu na uganga wa kienyeji kwenye mji wa Magdarena Mhoja walifika vijana wawili waliotambulika kwa majina ya Shigera Majinja (25) na Mhoja Shilinde (18) wakazi wa kijiji
hicho ambao walijifanya ni
wateja wake wa vyungu na kwa ajiri ya matibabu ya tiba za jadi
Alieleza ndipo walipoanza
kumhoji marehemu juu ya
mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja
na kutaka kujua mahari
ambapo marehemu alikokuwa akiishi na chumba alichokuwa akilala na alikuwa akilala na nani
Marehemu aliwajibu watu hao kwa
ufasaha bila kuwa na mashaka nao huku mazungumzo hayo yakiwa yanasikilizwa na Tausi Mlitoni ambae nae alikuwa kwenye eneo hilo
akiwa shahidi wa mazungumzo
hayo
Ailesama ndipo siku
hiyo ya desemba 29 majira
ya saa mbili na nusu asubuhi mke
wa Lameck Mboka Zamda Militone baada ya kuona mama mkwe amechelewa kuamka alienda kujaribu kufungua mlango na kukuta umefungwa kwa nje
Kidavashari alieleza
ndipo Zamda alipofungua
mlango huo wa chumba cha mama mkwe wake na kuingia ndani na alimkuta mama mkwe wake akiwa ameuwawa kinyama kwa
kukatwa mapanga kicwani na kwenye siko la lake kulia
Baada ya kuona hari hiyo ya
mauwaji ya kinyama alipiga mayowe na
majirani walifika kwenye eneo hilo la tukio na kujionea jinsi marehemu
alivyokuwa ameuwawa kinyama
Kamanda Kidavashari alisema
jeshi la polisi linawashikilia watu watatu kuhusiana na tukio hilo ambao
ni Shigera Majija (26) Mhoja Shilinde (18) na Masanja Ngasa (31) wakazi wa kijiji
hicho cha Kakese na mtuhumiwa wanee Walu Ngasa bado anaendelea kutafutwa
na polisi baada ya kukimbia
Kwa mmijibu wa
Kidavashari watuhumiwa
hao wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani baada ya
upelelezi wa tukio hilo utakapo kuwa umekamilika
No comments:
Post a Comment