Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi
wakiwa na silaha mbili bunduki aina ya
SMG wamemuwa kwa kumpiga risasi
mbili tumboni Juma Mabula ( 36) mfanyabiashara wa Bariadi
Shinyanga na kumpola
mamilioni ya fedha ambazo kiasi chake hakija fahamika na kumjeruhi
kwa kumpiga risasi mbili tumboni Cosmas Michael ( 28) mfanya
biashara wa Bariadi Shinyanga na kumpora fedha tasilimu milioni tatu
Kamanda wa polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alisema tukio hili lilitokea
juzi majira ya saa mbili usiku
katika kijiji cha Itunya
kata ya Kapalamsenga Tarafa ya Karema wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Alisema majambazi
hao kabla ya kufanya tukio hilo waliwavamia
Adolfu John (20 ) na kumpora
fedha tasilimu Tsh 4, 000, 000/= na Richard Charles (25) alimporwa
Tsh 5,000,000/= ambao ni wafanya biashara na wakazi wa
Kijiji cha Kakese Wilaya
ya Mpanda
Kidavashari
alieleza kuwa wafanya biashara hao walikuwa
wamekwenda kijijini hapo kwa lengo
la kununua zao la mpunga linalopatikana
kwa wingi kwenye kijiji hicho na ndipo
walipo patwa na tukio hili
Alisema katika
eneo la tukio hilo liliokotwa ganda moja
la risasi aina ya bunduki ya SMG
lililotumika likiwa karibu na
mwili wa marehemu Juma Mabula
Baada ya jeshi la
polisi kupata taarifa lilifika katika eneo hilo
la tukio na waliendesha msako
mkali na kuwakamata watu wanne kuhusiana na tuhuma za tukio hilo
Kamanda
Kidavashari aliwataja watu hao
wanao shikiliwa na polisi kuwa ni Mussa Mathias (36),
Ngusa Tola (37), na Shinde
Jiyaago ( 34) wote wakazi wa kijiji cha Nkuswe Tarafa ya Karema wilayani hapa
na Doto Kayungilo
(25) Mkazi wa kijiji cha Mnyamasi Tarafa ya Kabungu
Alisema majeruhi Cosmas Michael
ambaye amelazwa katika Hospital ya Wilaya ya Mpanda
anaendelea kupata matibabu na hali
yake inaendelea vizuri
Kamanda
Kidavashari amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwabaini wageni wanaofika kwenye maeneo
yao na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za kuwaarifu
watakao wabaini au kuwatilia shaka watuhumiwa ili waweze kukamatwa kabla ya kutenda tukio
No comments:
Post a Comment