Sunday, March 17, 2013

Polisi wakamata Pikipiki ya Bodaboda iliyoibiwa‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kukamata pikipiki
ya mwendesha bodaboda iliyo kuwa imeibiwa kufuatia msako
ulio fanywa na jeshi hilokatika mwambao wa ziwa Tanganyika
Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph Myovela alisema
jeshi hilo limefanikiwa kukamata pikipiki aina ya Sunlg yenye
namba za usajiri namba T695 mali ya Richald Julius iliyo ibiwa
wiki iliyo pita katika kituo cha bodaboda kilichopo katika
mtaamji mwema mjini hapa
Alisema mara jeshi hilo lilipo pata taarifa ya wizi huo
lilianza msako wa kumsaka wizi huyo kwa kushirikiana na vituo
vidogo vya polisi vilivyopo nje ya mji wa Mpanda
Myovela alieleza ndipo hapo juzi askari wa kituo kidogo cha
polisi cha Karema kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika ambao
walikuwa na taarifa ya kuibiwa kwa pikipiki walipo itilia
shaka pikipiki ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mtu wasie mfahamu
huku ikiwa haina pleti namba
polisi walimtaka mwendesha pikipiki huyo asimame na badala yake
aliamua kuitekeza pikipiki hiyo na kutokomea polini licha ya
askari polisi kumfukuza hakuewaza kufanikiwa kumkamkamata
Kaimu kamanda huyo wa polisi wa mkoa wa Mkoa wa Katavi alisema
kuwa hivi karibuni kumezuka wizi wa pikipiki katika mkoa huu
ambapo wezi hao wamekuwa wakisha kuziiba wanazipeleka kuwauzia
wavuvi wa samaki katika mwambao mwa ziwa Tanganyika ambao
wamekuwa wakitumia injini za pikipiki kuweka kwenye boti
zao za uvuvi na za kusafirishia abilia
Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limewataka waendesha pikipiki
wawe waangalifu na wachukue taadhali pale wanapo kuwa wanapaki
pikipiki zao ili kuepukana na wizi ulioanza kujitokeza kwa kasi
siku za hivi karibuni

No comments:

Post a Comment