Wednesday, February 13, 2013

MWENDESHA PIKIPIKI JELA KWA KUINGILIA MSAFARA WA PINDA‏


Na Walter Mguluchuma, Mpanda
Dreva maarufu wa pikipiki za abiria boda boda mjini Mpanda
Selemani (Baunsa) (35) amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela
kwa kosa la kuingilia msafara wa Waziri Mizengo Pinda wakati wa
ziara yake Mkoani Katavi
Hukumu hii ilitolewa hapo juzi na Hakimu mkazi mfawidhi wa
mahama ya ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa hukumu ambayo iligusa
hisia za watu wengi wa mji wa mpanda
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashita wa polisi Ally Mbwijo
aliiambia mahama kuwa Sele Baunsa alitenda kosa hilo la
kuingilia msafara wa hapo Demba 16 mwaka jana majira ya saa 11
jioni katika eneo la benki ya CRDB wakati waziri mkuu Mizengo
Pinda alipo kuwa akirejea nyumbani kwake Mtaa wa Makanyagio wakati
akitokea wilayani Mlele
Alieleza mahamani hapo pomoja na Semani kisimamishwa na askari wa
usalama barabarani ili aupishe kwanza msafara huu hakuweza kutii
agizo hilo na ndipo alipo ingiza pikipiki yake na kuanza
kupishana na msafara huo
Mwendesha mashitaka huyo alisema baada ya kutokea hari askari wa
usalama barabarani walianza kumfukuza na walifanikiwa kumkamata
hata hivyo aliwagomea kumpeleka kituo cha polisi kwa kile alicho
dai hawezi kwenda kituo cha polisi hadi hapo atakapo fika kamanda
wa polisi wa mkoa huo kwa kile alicho kidai askari wa usalama
barabarani wamemuonea
Kamanda wa mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari ambae nae alikuwa
kwenye msafara huo alifika kwenye eneo hilo na kuamuru mwendesha
pikipiki huyo ampelekwe kituo cha polisi agizo ambalo
lilitekelezwa na mshitakiwa alitii amrii hiyo
Karika kesi hiyo mwendesha mashitaka alimsomea mashitaka matano
mshitakiwa ambaye alifikishwa mahamani hapo kwa mara ya kwanza hapo
desemba 18 mwaka jana
mashitaka aliyo shitakiwa mahamani hapo ni kiendesha pikipiki akiwa
amelewa, kuingilia msafara wa Waziri Mkuu, kuendesha pikipiki bila
leseni , kuendesha pikipiki akiwa amelewa pombe na kusimamishwa na
polisi na kukataa kusimama
Hakimu Tengwa baada ya kusikiliza kesi hiyo alisema mahamani hapo
kuwa ameridhika na mwenendo wa kesi hiyo kwa ushahidi wa pande hizo
mbili za mashitaka na utetezi
Alisema mahakama imemuona mshitakiwa ana hatia hivyo kabla ya
kutolewa kwa hukumu inatowa nafasi kwa mshitakiwa ajitetee
Katika utetezi wake aliiomba mahakama imwachie huru kwani askari
wa usalama barabarani walimkamata kwenye eneo hilo kwa kumfananisha
aliye ingilia msafara hakuwa yeye bali ni mwendesha pikipiki
mwingine sio yeye
Hakimu Tengwa alipinga ombi hilo kwa kile alicho eleza kuwa mahakama
haiko tayari kuona watu wanashindwa kutii amri za usalama barabarani
na ndio imekuwa chanzo cha ajari za mara kwa mara na kusababisha
vifo vya watu kwa hari hiyo mahakama imetowa adhabu ya faini ya
shilingi 500,000 kwa Selemani au keanda jera miezi mitatu
Mshitakiwa alishindwa kulipa faini hiyo aliiliyo pelekea aende jela
kutumikia kufungo cha miezi mitatu jela katika gereza la mpanda mjini
mwisho

No comments:

Post a Comment