Na Walter Mguluchma-Blogs za Mikoa
Mpanda
Mahakama ya Hakimu mkazi ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu Shaban juma maarufu Mzigaba ( 31) mkzazi wa mtaa wa Nsemulwa kichangani mjini hapa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kujifanya afisa usama wa Taifa
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa na kuguza hisia za watu wengi wa Mji wa Mpanda na vitongoji vyake
Awali mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Razaro Masembo alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo katika tarehe tofauti hapo Aprili mwaka jana
Alidai kuwa Shabani katika kipindi hicho aliweza kujipatia kiasi cha fedha shilingi 315 000 baada ya kuwadanganya watu kuwa yeye ni afisa ulama wa Tajfa alitumwa na idara hiyo kuorodhesha majina ya watu wanao taka ajira ya utumishi katika idara ya TAKUKURU na idara ya usalama wa Taifa
Mshitakiwa baada ya kuwaorodhesha majina ya watu hao aliweza kuwadanganya wampe pesa ili aweze kuwapatia nafasi hizo za kazi na ndipo alipo weza kupatiwa na watu hao kiasi hiccho cha pesa
Mwandesha mashitaka Masembo aliileza mahakama mshitakiwa alikamatwa baada ya watu hao walio kuwa wamempa pesa kuona muda umekuwa mwingi huku hawaoni kilicho kuwa kinaendelea kuhusiana na ajira zao
Alisema watu hao ndipo walipo amua kwenda kutowa taarifa kwenye jeshi la polisi wilayani Mpanda na ndipo walipo anza msako na kufanikiwa kumkamata mshitakiwa Shabani
Alielezakuwa miongoni mwa watu walio danganywa na mshitakiwa ni watoto wa watumishi wa idara mbambali wa serikali wa wilaya hii pamoja na jeshi la polisi
Hakimu Chiganga baada ya kusikiliza maelezo ya pande mbili hizo za mashitaka na mshitakiwa aliridhika na na ushahidi ulio tolewa mahamani hapo na ndipo alipo alipo mtaka mshitakiwa ajitetee baada ya mahakama kumwona ana hatia
Mshitakiwa Shaban katika utetezi wake aliiomba mahakama imwachie huru kwa kile alicho kidai kuwa ushahidi ulio tolewa dhidi yake ulikuwa hauna ukweli wowote bali wamemsingizia tuu
Hakimu Chiganga aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amevunja sheria ya kifungu cha sheri ya Nchi namba 100 B cha kanuni ya adhabu cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002
Hivyo mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya hiyo imemtia hatiani Shaban Juma imemhukumu kifungo cha kutumikia jela miaka mitatu ili iwe fundisho kwa watu wengine wanye tabia ya kujifanya kuwa watumishi wa Serikali
Shaban baada ya kusomewa hukumu hiyo aliiomba mahakama impatie nakala ya hukumu iliaweze kwenda nayo gerezani ombi ambalo lilitekelezwa na Hakimu Chiganga kwa kumpatia nakala yake hiyo ya hukumu
No comments:
Post a Comment