Friday, February 15, 2013

AISHIA JELA MIAKA 30 BAADA YA KUBAKA


Na Walter Mguluchuma wa Blogs za Mikoa 
Mpanda
Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
imemuhukumu Pascal Fransisi (20) mkazi wa kijiji cha Igalula
kata ya Mpanda ndogo kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana
na hatia ya kubaka mwanamke kwa nguvu
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Mpanda Chiganga Tengwa baada ya kulidhika na
ushahidi wa mashitaka ulio tolewa mahakamani hapo dhidi ya
mshitakiwa
Awali mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alidai kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo februari 11 mwaka huu majira ya saa 10 kamili
jioni nyumbani kwake
Alieza kuwa siku hiyo Fransinsi akiwa nyumbani kwake alimbaka
mwanamke (21) mkazi wa kijiji cha Kambanga wakati akiwa anapita
eneo la nyumbani kwake
mwendesha mashitaka aliendelea kuileza mahakama kuwa pamoja na
mwanamke huyo kumkatalia kuingia ndani kwake Fransisi aliweza
kufanikiwa kumwingiza ndani ya nyumba yake kwa nguvu
Mshitakiwa baada ya kumwingiza ndani ya nyumba yake mwanamke huyo
alianza kumwingilia kwa nguvu kimwili licha ya mwanamke huyo
kupiga mayowe ya kuomba msaada Fransisi hakujali aliendelea tuu
kumfanyia unyama mwamke huyo
Hakimu Chiganga baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashitaka
na mshitakiwa alilidhika na ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo
na ndipo alipo mtaka mshitakiwa ajitetee kutokana na mahakama
kumwona mshitakiwa kuwa ana hatia
Mshitatakiwa Fransisi katika utetezi wake aliiomba mahakama isimpe
adhabu kutokana na kile alicho kieleza kuwa mwanamke huyo
walikuwa na mahusiano nae ya kimapenzi
aliendelea kujitetea kuwa mwanamke huyo aliamua kumshitaki baada
ya kuwa wamemaliza tendo la ndoa na yeye Fransisi kushindwa
kulipa pesa ndio akaamua kumsingizia kuwa amembaka kwa nguvu
Hakimu Chiganga ailiambia mahakama kuwa mshitakiwa amevunja sheri
ya kifungu namba 30 na 31 cha kanuni ya adhabu ya marekebisho ya
sheria ya mwaka 2002
kwa hari hiyo mahakama imemtia mshitakiwa hatia hivyo imemuhukumu
Fransisi kwenda jela kutumikia kifungo cha maaka 30 jela

No comments:

Post a Comment