Na Walter Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya msingi Itenka B wilayani mlele mkoa wa Katavi Peter Mabula (48) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jera kwa kosa la kupokea rushwa ya Tsh. 280,000
Hukumu hiyo imetolewa hapo jana na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya mpanda Chiganga Jengwa.
Katika kesi hiyo mwendhesha mashitaka wa PCCB Expediza Gwembe aliieleza Mahakam kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 3 mwaka 2010
Peter alidaiwa kuomba rushwa hiyo kwa Adamu Manjano ili aweze kumpatia ukandarasi wa kukaratabi nyumba tatu za walimu wa shule ya msingi Itenka B ukarabati ambao ungegharimu sh. Milioni 3,108,000
Gwembe aliieleza mahakama hiyo kuwa ndipo Peter alipomtaka mkandarasi huyo ampatie sh. 280,000 ili aweze kumpa tenda hiyo na kati ya fedha hizo yeye alidai apewe shilingi 100,000 na wajumbe sita wa kamati hiyo ya shule wapewe 180,000ili waweze kugawana sh. 30,000 kwa kila mjumbe.
Alidai mahakamani hapo kuwa Adamu alikubaliana na ombi hilo na ndipo kamati hiyo ya shule ikawa imempa tenda ya ukarabati wa nyumba hizo tatu za walimu .
Mwenyekiti huyo baada ya kuona kamati ya shule imempitishia tenda alimfuata mkandarasi huyo na kumtaka amptaie sh. 600,000 badala ya zile 280,000 walizokubaliana awali.
Mwendesha mashitaka aliendelea kuielezea Mahakam kuwa baada ya Adamu kuona kiwango kimekuwa kikubwa alichukua uamuzi wa kutoa taarifa PCCB.
Alieleza baada ya taarifa kufikishwa PCCB walianza kuandaa mtego wa kumkamata mwenyekiti huyo wa kamati ya shule.
PCCB walifanikiwa kumkamata Peter apo juni 3 2010 katika eneo la shule ya sekondari ya mwangaza eneo ambalo walikuwa wamekubaliana apokelee fedha hizo.
Gwembe alisema baada ya kupokea fedha hizo maafisa wa PCCB walimweka chini ya ulinzi mshitakiwa na walimpompekua na walipompekua walimkuta na fedha sh. 25,000 zilizokuwa zimeandaliwa na PCCB na walipozikagua kwenye fomu maalumu waliweza kuzitambua namba hizo
Hakimu Chiganga akisoma hukumu hiyo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa Peter amepatikana na hatia kwa kuvunja sheria 15(1) (a) namba 11 ya mwaka 2007
Hivyo mahakama inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jera kwa mshitakiwa Peter Mabula kukiuka sheria ya kupambna na rushwa
No comments:
Post a Comment