Na Walte Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Mkuu wa wilaya ya Nkasi ambae pia ni mlezi wa Klabu ya waandishi wa habari wa Rukwa na Katavi Iddy Kimanta amewataka waandishi wa habari kuandika zaidi habari zinazowahusu watu wenyewe wa vijijini
Ushauri huo aliutoa hapo janqa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Katavi kwenye ukumbi wa Dilux mjini Mpanda.
Kimanta alisema waandishi wa habari wanapoandika habari za vijijini wanachangia kwa kiasi kikubwa kichochea maendeleo ya vijijini ambapo taarifa za kazi mbalimbali za maendeleo zinazokuwa zikifanyika zimekuwa haziandikwi.
Alifafanua kuwa wananchi wa vijijini wamekuwa wakivunjika sana moyo pale wanapokuwa wamefanya jambo Fulani la maendeleo harafu linakuwa halitolewi na vyombo vya habari
Alieleza zinapoandikwa habari za vijijini kwenye vyombo vya habari vinawafanya hata wananchi wa vijiji vingine waige kilichofanywa na wenzao
Kimanta pia aliwataka waandishi wa habari kuandika habari zinazosaidia kufichua uozo mbalimbali unaofanywa na taasisi na serikali.
Hivyo pale wanahabari wanapoona mambo yanakwenda kinyume ni vizuri waandishi wayaweke wazi na pale panapokuwa yamefanyika mambo mazuri ya maendeleo yaandikwe pia.
Aidha Kimanta amewaomba viongozi wa serikali wawe tayari pale wanapokuwa wamekosea wanapa kosolewa
Alesema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa akiwachukia waandishi wa habari wanapokuwa wametowahabari zenye ukweli halisi unaokuwepo.
kwailo mkuu umenena kwani uku vijijin tunafanya mambo makubwa na mazuri lakini ayatangazwi
ReplyDelete