Na walter mguluchuma
Mpanda
JESHI la polisi Mkoani Katavi limefungua jumla ya kesi 7817 za makosa
mbalimbali
katika kipindi cha miaka miwili kuanzia January 2011 hadi Desemba 2012
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa wa
katavi Bw,Kidaua Shari alisema katika kipindi hicho kulitokea kesi
nyingi ambo ni mchanganyiko.
Alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia januari hadi Desemba mwaka jana
jumla ya kesi 3287 za makosa mbalimbali zilizofunguliwa na kesi 888 ndizo
zilizoweza kufikishwa mahakamani .
Hata hivyo alieleza kuwa kati ya kesi hizo zilizopelekwa mahakamani mwaka
jana ni kesi 349 ndizozilizosikilizwa na kumalizika.
Alisema mwaka 2012 kuanzia Januari hadi desemba kesi 4530 zilifunguliwa na
kesi 1049 ziliweza kufikishwa mahakamani na kesi 270 ndizo zilizoweza
kusikilizwa na kumalizika.
Aliongeza kuwa katika makosa hayo makosa makubwa ya mauaji yaliyookea mwaka
jana yalikuwa 88 na mwaka huu makosa yalikuwa60.
Alieleza kuwa makosa hayo makubwa yamekuwa yakisababishwa na wizi wa
mifugo ,sababu nyingine aliiyoitoa nitamaduni tofauti pamoja na imani za
kishirikina nakuongeza kipindi cha mwaka jana makosa ya unyang’anyi
yalikuwa 77 na mwaka huu ni makosa 70 yaliyofunguliwa mashitaka.
Kidaua shari alisema kuwa kesi nyingi zinazopelekwa mahakamani pamoja na
upelelezi ukiwa umekamilika na zile zinazochelewa kumalizika kutokana na
mahakama ya hakimu mkazi kuwa hakimu mmoja kwa Mkoa mzima.
Katika kuhakikisha jeshi hilo limeweza kuongeza ulinzi kwenye minada na
kwenye usafiri wa mabasi yanayoingia na kutoka ndani ya mkoa huo wa katavi
na kupunguza matukio hayo.
No comments:
Post a Comment