Sunday, November 25, 2012

MAHABUSU JELA MIEZI 6 KWA KUTOROKA MAHAKAMNI MBELE YA HAKIMU MKAZI‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda-Katavi
Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya yam panda imewahukumu kifungo cha miezi sita jela kila mmoja mahabusu wawili waliotimua mbio wakiwa mahakamani wakisubiri kesi zao.
Waliohukumiwa ni Jofrey masesha (35) mkazi wa Ikuba tarafa ya mpimbwe na John Gaudensi (30) mkazi wa Usevya wilaya ya Mlelel ambao wote walikuwa wametoka  gereza la mahabusu la wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kutajwa kesi zao.
mahabusu hao waliohukumiwa juzi na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Chiganga Tengwa.
John na Jofrey  katika tukio hilo ambalo lilitokea juzi majira ya saa 6:00 mchana walikuwa ni miongoni mwa mahabusu 40 waliokuwa mahakamani hapo wakisubiri kesi zao kusikilizwa na hakimu Tengwa.
mahabusu hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya wizi wa kutumia silaha, uvunjaji pamoja na kumiliki silaha aina ya Gobole kinyume cha sheria.
wakati Hakimu mfawidhi Tengwa akiwa anaendelea na kesi nyingine ya takukulu mahakamani hapo  iliyokuwa imevuta hisia za wasikilizaji pamoja na polisi walio kuwa wakiwalinda mahabusu ndipo mahabusu hao walipotumia nafasi hiyo ya kuruka ukuta wa mahakama na kutimua mbio.
polisi walipoona mahabusu hao wametimua mbio walianza kuwafukuza huku wakifyatua risasi hewani lakini mahabusu hao waliendelea kutimua mbio kuelekea eneo la shule ya msingi Kashaulili iliyoko jirani na mahakama.
wanafunzi baada ya kusikia milio ya bunduki walitoka madarasani shule nzima na ndipo walipowaona mahabusu hao wawili wakiwa wanakimbia.
hari hiyo iliwafanya wanafunzi waanze kuwafukuza huku wakiwashaumbulia kwa mawe na baada ya muda mfupi walifanikiwa kuwakamata na kuwakabidhi askari polisi.
baada ya kuwakamata mahabusu hao walipelekwa moja kwa moja mahakamani hapo huku wakiwa wanasindikizwa na umati wa watu wapatao 250
Hakimu mkazi Tengwa ambaye alikuwa anaendelea kusikiliza kesi nyingine mara walipofikishwa mahabusu hao alisimamisha kesi ambayo alikuwa akiendelea nayo na kuamuru mahabusu hao wapande kizimbani.
Kisha aliwaeleza mahabusu hao kuwa kwa kitendo chao cha kukimbia wakiwa chini ya ulinzi na huku mahakama ikiwa inaendelea hivyo wanatiwa hatiani kwa kosa la kuizuia mahakama ishindwe kufanya kazi zake.
Mahabusu hao waliiomba mahakama isiwape adhabu kwa kile walichokidai kuwa walifanya hivyo kwa kuwa wamekaa muda mrefu mahabusu  bila kesi zao kusikilizwa
Pia walieleza kushawishiana kutoroka kufuatia mahakama hiyo ya Mpanda kuwa na miundo mbinu mibovu inayofanya eneo kuwa rafiki kwa mtuhumiwa kimbia
Hakimu Tengwa baada ya kusikiliza utetezi huo alisema washitakiwa wanatiwa hatiani na wanahukumiwa kwa kifungu cha sheria No. 114 sura ya 16 majereo ya mwaka 2002 hivyo mahakama  inawahukumu kifungo cha miezi sita jera kwa kila mmoja.
watuhumiwa hao watafikishwa tena mahakamani wiki ijayo kujibu shitaka la kutoroka chini ya ulinzi

No comments:

Post a Comment