Monday, October 1, 2012

CCM MPANDA WAPATA VIONGOZI WAPYA‏

Na Walter Mguluchuma

Mpanda
Chama cha Mpanduzi (CCM) wilaya yam panda mkoa wa Katvi kimepata viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho kwa  kipindi cha miaka mitano
viongozi hao walipatikana hapo juzi kwenye uchaguzi uliofanyika katika shule ya sekondari ya milala
katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti  wa CCM Wilaya ya Mpanda BEDA KATANI aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti baada ya kupata kura 477 dhidi ya kura 208  alizopata mpinzani wake FORGENSIA KAPAMA
Nafasi ya Katibu mwenezi alichaguliwa JOSEPH LWAMBA aliyewashinda wapinzani wake wawili kwa kupata kura 59 nafasi ya pili alikuwa ni ELIAS MWANISAWA aliyepta kura 27 na watatu ni GENOVEVA MBAMBA  aliyepata kura 18
kwa upane wa mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa alichaguliwa Moshi Selemani Kakoso aliyepata kura 352 PIUS BUZUMALLE alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 235 na nafasi ya tatu ni GABRIE MNYERE aliyepata kura 85
mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya mpanda  pia umemchagua ALKADO KALIFUMU kuwa Katibu wa uchumi wa chama hicho wilaya yam panda.
mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo majira ya saa 8 usiku  wagombe wote waliochaguliwa na ambao hawakuchaguliwa walipewa nafasi ya kutoa maoni yao kwa wajumbe wa mkutano huo mkuu.
Wagombe hao kila mmoja alielezea kuridhishwa na matokeo hayo kwa kile walicho kieleza kuwa uchaguzi ulikuwa  ni wa haki.
baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wameilalamikia kamati iliyokuwa inasimamia chakula kwa kile walichodai kushindishwa na njaa kutwa nzima kwani chakula kwa wajumbe kilitolewa majira ya saa 4:00 usiku

No comments:

Post a Comment