Monday, September 3, 2012

WANANCHI WATIMUA MBIO MSIBANI BAADA YA WAGANGA WA JADI KUTOA MWILI WA MAREHEMU AKIWA NA SOKSI NA SURUALI KIFUA WAZI WAKIDAI KUMFUFUA

Walter Mguluchuma, Katavi Yetu

Wakazi wa Kijiji cha Kakese Wilayani Mpanda wamelazimika kukimbia mbio wakiwa msibani wakisubiria kuzika marehemu Sikitu mwinamila (40) baada ya waganga wa jadi wawili waliotokea Mkoani Shinyanga kumtoa marehemu huyo nje akiwa amevaa soksi na suluali wakidai kuwa wamemfufua.

Miongoni mwa waliotimua mbio msibani hapo ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mpanda Fredinand Filimbi na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM wa Wilaya yaMpanda Bw. Beda Katani.

Tukio hiilo lilitokea hapo juzi majira ya saa 9 Alasiri Nyumbani kwa mama mzazi wa marehemu huyo katika kijiji cha Kakese hapo Agosti 30 mwaka marehemu huyo ambaye alifariki katika Hospitari ya Wilaya ya Mpanda kutokana na ajari ya pikipiki iliyotokea siku moja kabla ya kifo chake katika eneo la mkwajuni kata ya Kakese.

Baada ya marehemu Sikitu kufariki ndugu zake walitoa taarifa kwa baba yake mzazi wa marehemu aitwaye Lumba Mwinamila ambaye alikuwa safarini Mkoani Shinyanga.

Lumba baada ya kupatiwa taarifa za msiba wa mwanae aliagiza marehemu asizikwe mpaka yeye atakapo kuwa amefika akiwa na Waganga wa jadi wawili kwa kile alichodai kuwa mwanae hajafa wanakuja kumfufua.

Ndipo siku ya Jumamosi walipo wasiri Mjini Mpanda na kuelekea moja kwa moja Msibani na walipofika msibani walikuta waombilezaji mbalimbali na ndipo walipo mwona mama mmoja aitwaye Magdalena Kazibya (55) kisha walianza kumshambulia kwa kichapo wakadai ni mchawi na kumfanya mama huyo kuokolewa na waombolezaji na baada ya hapo walimfukuza Mke Mkubwa wa marehemu aitwaye Helena Jackson (33) kuwa nae hatakiwi kuwepo Msibani hapo.

Kufuatia tuko hilo Ndugu wamarehemu walipanga kufanya mazishi ya marehemu Sikitu siku ya Juma Pili yaani Juzi majira ya saa sita mchana kuwa ndio muda wa mazishi na kisha waliandaa utaratibu wa kwenda kuuchukua mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitari Wilayani Mpanda siku hiyo ya mazishi.

Viongozi wa Dini wa Kanisa la AIC alikokuwa anasalia marehemu walipewa taarifa za utaratibu huo na waso wakaandaa utaratibu wa kumfanyia ibada mara mwili huo utakapo kuwa umewasiri kijijini hapo kwa ajili ya mazishi.

Hata hivyo ndugu wa marehemu waliwakatalia Viongozi hao wa dini kufanya Ibada kwa kile walichokieleza wanamfanyia shughuli za ki mila marehemu huyo kabla ya kumzika na kuwafanya viongozi hao wa Dini wakasirishwe na kuamua kuchukua vitabu vyao vya kuendeshea ibada

ndipo waganga hao wawili ambae mmoja alijitambulisha kwa jina moja la Tatu pamoja na baba mzazi wa marehemu waliingia ndani ya chumba alichokuwa amehifadhiwa marehemu akiwa ndani ya sanduku

waombolezaji walipoona muda unazidi kwenda ambapo walikua wametaarifiwa mazishi saa sita mchana hadi muda huo wa saa tisa hakuna dalili zozote za kumzika marehemu walianza kuuliza kulikoni ndipo baba mzazi wa marehemu alipotoka na kuwaambia mwanae wanamtoa nje waganga muda si mrefu

kisha si muda mrefu waganga hao wawili wa kike wakiwa na baba mzazi walitoka na marehemu wakiwa wamemshikilia huku akiwa amevaa soksi na suruali akiwa kifua wazi hali iliyofanya waombolezaji waliokuwa hapo wengi wao kutimuwa mbio na kuelekea kusiko julikana na wengine ambao hawakuwa katika eneo hilo waliweza kusogea ili kushuhudia kuna nini

bado waganga hao walimsimamisha marehemu sikitu huku wakiwa wamemshikilia na mganga Tatu akiwa ameshika mkia wa ngombe akinyunyizia dawa katika eneo hilo na kisha alianza kuwatolea kauli wananchi waliokuwa wamekusanyika eneo hilo kuwa watoke ili sikitu aweze kupata hewa

ndipo baada ya muda walimchukua tena marehemu sikitu na kumrudisha ndani na kisha kuwatangazia wananchi kuwa wamefaulu kuurudisha mwili wa marehemu sikitu kuwa mwili wa binadamu baada ya kubadilishwa kuwa ni mwili mbwa hata hivyo kitendo hicho kiliwakasirisha baadhi ya waombolezaji kwa kile walichokieleza kuwa waganga hao wameudhalilisha mwili wa marehemu na wao ndio wamzike hata hivyo baadhi ya watu wachache waliweza kufanya kazi ya kumzika katika eneo lililokuwa limeandaliwa nyumbani kwa mama yake mzazi

baada ya mazishi mwanasheria wa kujitegemea wa haki za binadamu Kisundwa wa marwa aliwataka waganga hao wawili na baba mzazi wawaeleze waombolezaji ni kwa nini wamefanya kitendo hicho cha uchonganishi katika jamii na kuleta chuki

walianza kujieleza kuwa wao ni wakazi wanatoka kijiji cha Luhumbo kata ya Itwangi wilaya ya shinyanga vijijini na ni waganga wa jadi na walikua wamekuja kumfufua marehemu sikitu baada ya kuombwa na baba mzazi wa marehemu waliekuwa nae kijijini hapo

kufuatia kauli hiyo wananchi walikasirika na kutaka kuanza kuwashambulia kwa mawe hali iliyopelekea Afisa mtendaji wa kata hiyo ya Kakese Ruben Kasomo kutoa ripoti kwa jeshi la polisi ambao walifika katika eneo hilo muda mfupi tu na kukuta waganga hao wamezingirwa na wananchi waliokuwa na hasira

afisa mpelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Katavi aliwahakikishia wananchi hao kuwa marehemu kwa taarifa za kidaktari baada ya kufanya uchunguzi zilibaiini kuwa marehemu kifo chake kilitokana na kuvuja damu nyingi na sio sababu nyingine na kisha aliwachukua waganga hao na kuwapeleka kituo cha polosi Mpanda mjini ambapo bado wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo.

Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment