Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kitoa heshima za mwisho kwa marehemu Mhashamu, Askofu Pascal William Kikoti katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa kuu katoliki, jimbo la Mpanda, Septemba 1, 2012.
Mapadri wakiweka kaburini mwili wa aliyekuwa Askofu wa jimbo la Mpanda Mhashamu Pascal William Kikoti kaburini katika mazishi yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la jimbo Katoliki la Mpada Mjini Mapanda Septemba 1, 2012
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitupa mchanga kwenye kaburi la Askofu Pascal William Kikoti katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Katoliki jimbo la Mpanda mjini Mpanda Septemba 1, 2012.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
****************************
Na Walter Mguluchuma
Mpanda.- Katavi yetu blog
Aliyekuwa Skofu Jimbo Kanisa Katoriki Jimbo la Mpanda marehemu Pascal Kikoti aliyefariki August 28 kutokana na ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando amezikwa leo katika Kanisa lake la Kiaskofu la Palokia la Maria Emakulata la Jimbo la Mpanda.
Katika mazishi hayo ambapo Serikali iliwakilishwa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mazishi ambayo pia yalihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mikioa ya Katavi na Rukwa wakiwemo Wakuu wa Mikoa hiyo na wabunge wa mkuo wa katavi.
Ibada hiyo ya mazishi iliongozwa na kadinari wa kanisa katoriki Porkapo Pengo, pia alikuwepo Rais wa baraza la Maakofu Tanzania, Taasisius NgalaleKumtwa Barozi wa Vatcan Nchini Tanzania na maaskofu 27 kutoka majimbo mbalimbali hapa Nchini.
Katika ibada hiyo Kadinari Pengo alieleza marehemu Askofu Kikoti katika uhai wake alitoa mchango wa huduma zilizo lenga kuwaletea wananchi maendeleo kwa ujumla.
Aliwaomba wananchi na waumini wa kanisa katoriki jimbo la Mpanda waakikishe wanaendeleza mipango ya maendeleo aliyokuwanayo hayati kikoti.
Kadinari Pengo alieleza kuwa yeye kama kiongozi wa Kanisa analifahamu vizuri sana Jimbo la mpanda na lilikuwa liko chini sana lakini kutokana na moyo ya kupenda maendeleo aliyokuwa nayo marehemu Askofu kikoti ndio umesababisha Jimbo hili la mpanda kupiga hatua kubwa tofauti na lilivyokuwa awali.
Kwa upande wake Raisi wa baraza la Maaskofu Taasisius NgalaleKumtwa Alisema marehemu Kikoti atakumbukwa na Baraza zima la maaskofu na watanzania kwa ujumla kutokana namoyo wake wa upendo aliokuwa nao na mshikamano kwani alipenda zaidi kutenda kuliko kusema.
Alieleza ndio maana muda mwingi sana marehemu Askofu Kikoti alipenda kuwatumikia Watanzania hali hiyo ndio iliyo pelekea kuleta huduma za jamii kwa wananchi wa Jimbo la Mpanda kama vile Kufungua Sekondari, Shule ya chekechea, Vitua vya Afya na zahanati panoja na huduma za maji na ujenzi wa seminari ndogo ambayo ameiacha ikiwa katika hatua za mwisho.
Nae mwakirishi wa Serilikari kwenye mazishi hayo waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alisema Serikali kwa Ujumla imefadhaishwa sana na msiba huyo mkubwa tena uliotokea kwa ghafla.
Pinsa alisema kuwa watu wote ni mashahidi wa mchango mkubwa wa marehemu mhashamu Askofu Kikoti alioufanya uinjirishaji hapa Jimboni mchango wake umegusa jamii nzima sio tu katika kutoa hujuma za kiroho bali pia huduma za jamii zilizolenga kuleta maendeleo kwa wananchi katika jimbo la mpanda na nchni kote kwa ujumla.
Mimi binasfi nimefanya kazi kwa karibu sana na mhashamu Askofu kikoti toka alipowekwa wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa jimbo la Mpanda mwaka 2001 nilifarijika sana kwa uongozi wake, maono yake na shauku yake ya kutoa huduma za kiroho na za kijamii kwa ujumla hivyo basi ni dhahiri kwamba kifo chake ni pigo kubwa sio kwangu au kwa waumini wa kanisa katoriki bali nikwa wananchi wa nchi nzima.
Barozi wa vatcan Nchini tanzania Fransisco alitangaza uteuzi wa Askofu wa jimbo wa Sumbawanga Damiani Kiaruzi kuwa Baba Matkatifu Benedicto hapo jana amemteua kuwa msimamizi wa Jimbo la Mpanda mpaka hapo atakapo kuwa ameteuliwa askofu mwingine hivyo jimbo hilo litakuwa chini ya askofu huyi wa Jimbo la Sumbawnga.
Barozi wa Vatcan alisema uteuzi huo umefanywa na Papa Benedcto wa Kumi na sita hapo August 31 ambapo nae Askofu Damian Kiaruzi alimteua na kumtangaza aliyekuwa msaidizi wa marehemu Askofu Pascal Kikoti Padri Patrick Kasomo kuwa ndiye atakaye kuwa msaidizi wake (Vikagenero)
No comments:
Post a Comment