Na walter mguluchuma
Katavi
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injiri hapo nchini Boni Mwaitege ameuteka mji wa mpanda kufuatia maelfu ya wakazi wa mji huo na vijiji vya jirani kufurika kwa wingi kwenye mkutano wa injiri
Mkutano huo wa injiri ulifanyika hapo jana katika uwanja wa shule ya msingi kashaulili uliopo mjini mpanda na kuhudhuriwa na na umati mkubwa sana wa wanachi wa madhehebu mbali mbali za dini za kikristu na za kiislamu
Wakazi hao walijitokeza kwa wingi kutokana na wengi wa wakazi wa mji wa mpanda kuwa na shauku ya kumwona mwaitege ambaye wamekuwa wakimwona kwenye tv na kwenye radio mbalimbali
Mwimbaji huyo aliamsha shamra shamra katika uwanja huo pale alipo simama jukwaani na alipo weza kutambulishwa
Mara alipopaanza kuimba wimbo wake maarufu wa mtamtambuaje mtu aliye okoka umati mzima ulilipuka kwa kucheza na wengine kumshangilia
Hii ni mara ya kwanza kwa mwaitege kuimba nyimbo za ijiri katika mkoa wa katavi na leo atafanya mkutano wa kutumbuiza nyimbo za ijiri katika uwanja huo hoo wa kashaulili mjini mpanda
No comments:
Post a Comment