Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi, Injinia Emmanuel Kalobelo, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Viongozi watatu wa ngazi ya juu wa serikali wa mkoa wa Katavi wametapeliwa baada ya kuambiwa wameshinda promosheni ya Airten ya milioni 50
Viongozi walitapeliwa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Rajabu Rutengwe, Katibu Tawala wa Mkoa Injinia Emmanuel Kalobelo na Mganga Mkuu wa Mkoa Yahaya Hussein
Viongozi hawa watatu walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa njia ya simu kuwa ni watumishi wa kampuni ya simu ya Airtel
Tukio la kwanza lilikuwa ni la Mkuu wa Mkoa kuambiwa ameshinda zawadi ya milioni 50 na kisha aliombwa awatumie namba za simu za watu watano alioongea nao mara ya mwisho na mara baada ya kufanya hivyo simu yake ya mkononi ikafungwa na matapeli hao
Akieleza mkasa huo mganga mkuu wa mkoa wa katavi Dk. Yahaya alisema yeye baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana ba kauli yao ilivyokuwa ya kistaarabu
Alisema baada ya kuwapa majina aya watu watano aliongea nao mara ya mwisho kwenye simu yake aliombwa awatajaie namba zake za siri za akaunti ya benki ya NMB ili wamatumie zawadi ya milioni 50
Baada ya kuombwa namba yake ya siri Dk. Yahaya hakuwa na shaka lolote na ndipo alipowapatia namba hiyo ya siri
Hata hivyo hakuweza kuibiwa pesa zozote kutokana na akaunti yake haikuwa na salio la kutosha
Aidha meneja wa tawi la NMB Wilaya ya Mpanda Erick Luhanda alisema amepokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao wa serikali wa mkoa wa katavi
Alisema kiongozi wa mwisho kumpa taarifa alikuwa ni katibu tawala wa mkoa Injinia Kalobelo hata hivyo tayari taratibu za kibenki zimefanyika hivyo hakutakuwa na hujuma itakayofanyika kwenye akaunti za viongozi hao.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa matukio hayo.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment