Home » » WARATIBU WA TASAF WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA WANDISHI WA HABARI.

WARATIBU WA TASAF WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA WANDISHI WA HABARI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

    Na  Walter Mguluchuma.
           Katavi 
Waratibu wa  TASAF  wa  mpango katika   ngazi  ya  Mkoa ,Halmashauri ,Maafisa  ufuatiliaji  wa   mpango na  Wandishi wa  Habari  katika  Mkoa wa  Katavi wametakiwa  kufanya kazi kwa ushirikiano  ili  kuhakikisha  kuwa wanatangaza  na kuelimisha  wananchi  kuhusu   malengo ya  mpango  wa  TASAF .
Wito  huo ulitolewa    hapo   jana  na    Mkuu wa   Mkoa wa  Katavi    Meja    Generali  Raphael   Muhuga   katika   hotuba  yake  ilisomwa kwa  niaba  yake   na   Kaimu  Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi    ambae   ni  Mkuu wa  Wilaya ya   Mpanda   Lilian  Matinga   wakati wa ufunguzi wa  mafunzo  ya kuwajengea uelewa  Wandishi wa   Habari wa  Mkoa wa  Katavi kuhusu  mpango wa   kunusuru   Kaya  maskini   yaliofanyika katika ukumbi wa Kichangani   Mjini  hapa .
Alisema  mafunzo  hayo  yatawapa   furusa   Wandishi wa   Habari  ya kupata  taarifa  za  maendeleo  ya utekelezaji  wa  Mpango  katika   Mkoa wa  Katavi  na  kufahamu    dhana   mbalimbali  za   mpango  wa  Tasaf   katika   Mkoa  huo .
Aliwasisitiza   Waratibu wa  mpango wa   Tasaf  na  wahasibu  wa  Halmashauri  kuhakikisha  kuwa  nyaraka  zote muhimu  za mpango  zikiwemo    nyaraka za  malipo  zilizopo   Halmashauri   nakala zake  zinakuwepo pia  katika   Vijiji na Mtaa inayotekeleza  mpango huo.
Pia  alizitaka  kila  Halmashauri  ijiwekee   mkakati  wa kuwahamasisha  wanufaika  wa  mpango  wa  Tasaf  wanajiunga na  mfuko  wa   Afya ya   jamii.
  Aliwaomba  Wandishi wa   Habari  washirikiane  kwa pamoja  kutangaza  utekelezaji  wa  Mpango wa  Tasaf katika   Mkoa huo  kwani  mambo mengi  mazuri  yanafanyika  lakini   hayatumiki  kuwasaidia  watu  wengine  wajifunze  kutokana  na   mpango wa  Tasaf.
  Hivyo ni  matumaini yake  kuwa  waratibu wa    mpango  katika   ngazi ya   Mkoa   na  Halmashauri  watawatumia  wandishi wa  Habari  katika  ziara zao  watakazo fanya  ili   kuweza  kuutangaza    mpango huu.
Mwakilishi wa  Mkurugenzi  Mtendaji wa  Tasaf   Zuhura   Mdungi  alisema   Tasaf   awamu  ya tatu  inatekeleza   mpango  wa  kunusuru   kaya  maskini   ambao  unawezesha   kaya  zilizoandikishwa  kupata  ruzuku  ili  kumudu   mahitaji ya  msingi  kama   elimu ,afya  na  lishe  na kuwekeza   katika  miradi  ya  ujasilimali .
Alifafanua  kuwa    madhumuni ya    mpango  ni kuziwezesha   kaya   maskini  kuwa  na  uhakika  wa  chakula ,kujenga  rasilimali ,   watoto  na  kutoa  fursa  kwa  kaya  kuongeza  kipato .
Mraribu wa   Tasaf wa   Mkoa  wa  Katavi   Ignas   Kikwala    alieleza kuwa  mafunzo  hayo  yatawajengea  uwezo wandishi  wa uwelewa  wa  pamoja  wa  masuala  muhimu  kuhusu   mpango  wa kunusuru    Kaya  maskini  na  kupeana  taarifa  za utekelezaji kwa  wandishi wa  habari  ili  waweze kupata wigo  mpana  wa  kutangaza  utekelezaji  wa   Mpango wa   Tasaf katika  Mkoa  huu.
 Alisema  Mkoa wa   Katavi  una vijiji  177 ila   vijiji  vinavyotekeleza    mpango wa   Tasaf   awamu ya  tatu  vipo 80 kwa  mwaka 2014    Mkoa  ulikuwa  na  kaya  8,537 zilinufaika na  mpango  huu  kwa sasa  zimebaki   kaya  7,668 .
  Kaya   hizo    zimepungua  kutokana  na  sababu    mbalimbali  ikiwemo  kwa  kaya ,kufariki  kwa wanufaika  wa  mpango ,,baadhi ya   kaya  kupata    nafasi  za uongozi  katika  Serikali  za     vijiji  Mtaa na  wengine kuondolewa kwa kukosa  sifa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa