Home » » MAJAMBAZI WAVAMIA MGODINI WAUA WAPORA DHAHABU NA FEDHA KWA KUTUMIA BUNDUKI KALI YA KIVITA

MAJAMBAZI WAVAMIA MGODINI WAUA WAPORA DHAHABU NA FEDHA KWA KUTUMIA BUNDUKI KALI YA KIVITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 

MASUNJU  MGELU  AKIWA  AMELAZWA KATIKA  HOSPITALI YA MANISPAA YA MPANDA BAADA YA KUPIGWA RISASI YA MGUU WAKE WA KUSHOTO   NA  MAJAMBAZI WATATU WALIOVAMIMIA  MACHIMBO YA  DHAHABUHUKO  ISUMAMILOMO KWA KUTUMIA  BUNDUKI YA KIVITA AINA YA AK  47  AMBAPO KATIKA TUKIO HILO  MCHIMBAJI MMOJA  ALIUAWA KWA KUPINGWA  RISASI TUMBONI NA WATATU KUJERUHIWA  AMBAPO  MAJAMBAZI HAO WALIPORA DHAHABU  GRAMU 650,MASHINE  MBILI ZA KUTAFUTIA  DHAHABU NA   FEDHA TASILIMU TSHS 1,500,000
PICHA  NA  WALTER  MGULUCHUMA-KATAVI YETU
Na  Walter  Mguluchuma .
    Katavi .
  Watu  watatu  wanaosadikiwa  kuwa ni  majambazi wamevamia   machimbo ya   madini ya   dhahabu  ya   Ifumile  Kijiji  cha  Isumamilomo  Tarafa ya  Nsimbo  Wilaya ya  Mpanda na kuuwa    mchimbaji   mmoja kwa  kumpiga   risasi tumboni  kwa  kutumia    bunduki ya   kivita  na  kujeruhi wengine watatu katika sehemu zao    mbalimbali za  mwili na  kisha  kupora   dhahabu ya  zaidi  ya   Gramu 600,fedha  tasilimu  Tshs  1,500,000 na   mashine  mbili za kutafutia  dhahabu .
  Kamanda  wa   Jeshi la  Polisi wa  Mkoa  wa  Katavi  Damas  Nyanda   aliwaambia  wandishi wa  Habari  kuwa  tukio  hilo la  ujambazi  lilitokea  hapo juzi  majira ya  saa  saa  mbili  usiku  katika  machimbo  hayo ya  madini ya  dhahabu .
 Alisema  siku  hiyo ya  tukio  majambazi hao  waliokuwa  watatu   walifika  katika  machimbo  ya  dhahabu ya  Ifumile yaliko  katika  Kijiji  cha  Isumamilomo  huku  wakiwa  wamejifunika  sura  zao   usono  KININJA   na  kuwashambulia  kwa risasi  za  moto  wachimbaji na  wanunuzi wa  dhahabu  kwenye  machimbo  hayo .
  Katika   shambulio  hilo   waliweza  kuwajeruhi vibaya kwa   risasi   wachimbaji wanne  katika   sehemu  zao   mbalimbali  za  mili yao   huku   baadhi ya  wachimbaji  walikuwa  kwenye    eneo  hilo  waliweza  kusalimika  baada  ya kuwa  wamekimbilia  kwenye  vichaka .
  Kamanda  Nyanda  aliwataja    majeruhi   walijeruhiwa kwa  kupigwa  risasi  kuwa  ni     Sita   Kalyalya   34  Mkazi wa   Bariadi  Shiyanga   ambae  alipingwa  risasi ya  tumboni   na  mkononi  aliyefariki Dunia   muda  mfupi  baada ya  kufikishwa katika  Hospitali ya  Manispaa ya   Mpanda  wakati    akiwa   anapatiwa  matibabu .
Wengine  waliojeruhiwa  ni   Joseph   Panya    34    ambae   amereruhiwa  vibaya  kwenye      bega  la  kushoto  na    mguu wa kulia    Mrisho   Rashid  21   aliyejeruhiwa   mguuni  na     mkono  wake wa kulia  na Masunju  Mgulu  28  aliyejeruhiwa     mguu na  mkono wake  wa  kushoto .
  Kamanda   Nyanda  alisema  majambazi hao watatu hao  baada ya  kuwajeruhi  wachimbaji hao  waliweza   kupora  fedha   tasilimu   Tshs  1,500,000    Gramu  650 za  madini ya   dhahabu  na  masine  mbili za  kutafutia  madini   na  kicha  walitokomea  kusiko julikana.
  Mara  baada ya tukio  hilo  polisi  walifika  kwenye   eneo  hilo  hata  hivyo  waliweza  kuokota   Risas  24 za  moto  na   maganda        saba  ya  risasi zilizotumika   za   bunduki ya  kivita   iliyotumika  kwenye  tukio  hilo    aina  ya   AK    47.
  Alisema   Jeshi la  polisi  Mkoa  wa  Katavi  bado  linaendelea  kuwasaka    majambazi waliohusika  kwenye  tukio  hilo  na   wametowa  wito kwa  wananchi  kutowa  ushirikiano kwa  jeshi  hilo  kwa  kuwapatia  taarifa  zitakazowawezesha  kuwatia  nguvuni  watuhumiwa  watukio  hilo .
  Kaimu   Mganga  Mkuu  wa  Hospitali ya  Manispaa ya  Mpanda  Dr    Masanja  alisema  marehemu   Sita    Kalyalya  alifariki muda  mfupi  baada  ya  kuwa   ametolewa kwenye chumba  cha upasuaji  ambako   alikuwa   akipatiwa  matibabu ya   kuunganishiwa  utumbo  wake  mkubwa   ambao  ulikuwa  umekatika  kutokana  na  kupigwa  risasi  tumboni .
  Alisema  majeruhi    Joseph  Panya   na   Mrisho  Rashid hao   ambao  walikuwa  wamelazwa  katika  wodi  namba  moja wamepewa  rufaa na  wamesafirishwa  kwenda  katika  hospitali ya  Rufaa ya  Muhimbili  kwa  ajiri ya  matibabu  zaidi  baada  ya hari zao kuwa  mbaya sana  ambapo  majeruhi Masunju   Mgelu  yeye   amebaki  kwenye  hospitali  hiyo  huku  hari yake  ikiwa  inaendelea  vizuri.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa