Home » » WAWILI MIAKA SABA KWA KOSA LA KUMILIKI SIRAHA AINA YA GOBOLE,RISASI 19 NA VIRIPUZI VYA 100KG

WAWILI MIAKA SABA KWA KOSA LA KUMILIKI SIRAHA AINA YA GOBOLE,RISASI 19 NA VIRIPUZI VYA 100KG

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter  Mguluchuma.
Mlele



WAKULIMA wawili wa kijii cha Majimoto , John Kalikwenda (50) na Kapufi Mdagula (40) wamehukumiwa  kila mmoja wao kutumikia kifungo cha miaka saba jela  baada ya kukiri  kupatikana na silaha aina ya gobole , risasi zake 19 na vilipuzi nyenye uzito wa kilo 100 .


Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi , Teotimus Swai katika  kosa la kwanza la kukutwa na silaha kila mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huku kosa la pili la kukutwa na risasi 19 kila mmoja  alihukumiwa kutoa faini  ya Sh 500,00/-.


Hakimu Swai katika kosa la tatu la kukutwa na vilipuzi  kila mmoja wa washtakiwa hao alihukumiwa kwenda jela  miaka saba au kkulipa faini ya Sh  milioni moja .


“ Kwa kuwa adhabu hizo zinaenda kwa pamoja  kila mshtakiwa  atatumikia kifunga jela  miaka saba au kulipa faini ya Sh milioni moja …. Mahakama  hii imetoa adhabu kali  ili iwefundisho kwa wengine wenye  tabia kama zao “ alieleza.
Hata hivyo washtakiwa hao wameanza kutumikia adhabu hiyo baada ya kushindwa  kulipa faini hiyo .


Awali Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Bahati Hongoli alidai mahakamni hapo kuwa washtakiwa hao wawili walitenda kosa hilo Aprili 27, mwaka huu saa nane mchana ambapo walikamatwa wakiwa ndaji ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Rukwa – Lwafi iliyoko wilayani Mlele .


Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei ,3,2017.
Mwisho



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa