Home » » MASHEKHE WATANO WAJIONDOA UONGOZI WA BAKWATA WA MKOA WA KATAVI .

MASHEKHE WATANO WAJIONDOA UONGOZI WA BAKWATA WA MKOA WA KATAVI .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma .
   Katavi .
Mashekh  watano  kati ya  sita wanaunda    baraza la    Halmashauri ya  Bawata ya  Mkoa wa  Katavi wametangaza kujiuzuru nafasi hiyo kwa  kile walichodai  kuwepo kwa mingongano ya uongozi na ukiukwaji wa   katiba ya  Bakwata .
Mashehke  hao walitangaza  hatua yao ya kuziuzu  hapo  jana  katika  kikao chao na  wandishi wa  habari  kilichofanyika  hapo  jana    mjini  hapa   na kuhudhuriliwa na   Mwenyekiti wao  Shekh  shaban  Bakari .
  Waliotangaza  kujiuzuru ni  Shekhe  Mashaka  Nassoro  Kakulukulu,  Shekhe  Hassani  Mbaruku,  Said  Hruna  Omary ,  Mohamed  Shabani  Sigulu  na  Mwenyekiti wao wa  baraza la   Halmashauri ya Bakwata   Mkoa wa  Katavi .
  Kwa  upande  wake  Shekhe   Mashaka Nassoro  Kakulukulu  alisema  yeye  haoni   sababu ya  kuendelea   na  nafasi  hiyo   kwa  kile   alichodai  kuwa  kumekuwepo na  baadhi ya  mambo ya kimaendeleo  yemekuwa  hayaendi sawa  ndani ya uongozi wa  Bakwata  Mkoa wa  Katavi .
 Alisema  kuwa  hata  katiba ya  Bakwata  imekuwa  ikikiukwa na  kumekuwepo na mgongano wa  baadhi ya maamuzi yanayotolewa  na  vikao  halali vya kuleta  maendeleo na  kutenguliwa  na  vikao  visivyo  halali  kwa  mujibu   wa  katiba ya  Bakwata .
Shekhe  Said   Omary  alisema  yeye  sababu kubwa  ilimfanya   achukue uamuzi huo wa kujiuzuru  ni  kutokana  na  mazingira  ya  viongozi wa  Bakwata kutofuata   Katiba .
Mohamed   Shaban  Sigulu    alisema   yeye   ameamua  kujiuuzuru kutokana na  uongozi wa  Bakwata kuwa na  msuguano    hari   ambayo imefanya  hata  miradi  ilipo  kusimama   kutokana na  msuguano wa kiuongozi .
  Alifafanua  kuwa  msuguano  huo uliopo  ndani ya  Bakwata umesababisha   hadi   mwalimu wa   madras I  katika msikiti  mkuu wa  Mkoa wa   Katavi kuamua kuacha kazi  hiyo  hivi  karibuni.
Mwenyekiti wa  Baraza  la   Halmashauri ya  Bakwata wa  Mkoa  Shaban  Bakari  alisema  ameamua  kujiuzuru  nafasi  hiyo  kwa   ajiri ya  kuwepo kwa  msuguano  ndani ya uongozi wa  Bakwata  Mkoa  hari  ambayo imekuwa  ikisababisha  baadhi ya vikao kufanyika  bila kuwepo kwa  wajumbe  halali wa vikao husika .
  Hivyo     yeye  haoni    tena  sababu ya   yeye kuendelea  kuwa     Mwenyekiti na   badala yake   anaona ni  vema  watafute     mtu   mwingine   afanye  kazi  hiyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa