Home » » CCM KATAVI WAPATA MWENYEKITI MPYA WA MKOA

CCM KATAVI WAPATA MWENYEKITI MPYA WA MKOA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Na  Walter  Mguluchuma.
     kATAVI

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa  (CCM) wa   Wilaya ya  Mpanada mkoani   Katavi   Beda  Katani  amechaguliwa  kuwa  Mwenyekiti wa  CCM  wa  Mkoa wa  Katavi  baada ya kushinda  mgombea   mwenzake  kwenye  nafasi hiyo  Enock  Gwambasa  ambae  aliwahi kuwa  meya wa  Manispaa ya  Mpanda .

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi ,    Deo  Njinjimbi alimtanga Katani   kuwa  Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa   Katavi  baada ya  kuchaguliwa  na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa wa  katavi uliofanyika jana na matokeo kutangazwa  jioni  mjini  Mpanda.

Katika uchaguzi huo  Beda  Katani ” alipata kura 304 , huku mpinzani wake  Enock  Gwambasa  akipata kura   46 nafasi hiyo ya  Mwenyekiti wa  CCM   wa    Katavi ilikuwa na wagombea wawili tuu .
Mkutano huo   Mkuu wa  CCM wa  Mkoa  ulimchagua  pia Gilbelti  Sampa  kuwa   mjumbe wa  Halmashauri  kuu ya Taifa ya  CCM NEC  baada ya  kuwashinda  wagombea  watatu wanafafi  hiyo .
Sampa  alishinda  baada ya kupata  kura   182,   na  wagombea  wenzake    walipata  Wense  Ka mtoni  kura , 157,  Hassanal  Dalla  kura  66  na  Alkado   Kalifumu  kura   4.

Aidha Halmashauri Kuu wa CCM mkoa wa   Katavi  ikiongozwa na mwenyekiti wake  mpya ,  Beda  Katani  ilimchagua  Jackoson  Lema kuwa Katibu Mwenezi CCM mkoa wa Katavi ambaye alifanikiwa  kupata  kura   24. na  kumshinda  mgombea  mwenzake    Linus  Kasakabaya  alipata kura   12.
Katika  hotuba  yake    mbele ya  wajumbe  wa  Mkutano  mkuu   Mwenyekiti  huyo   mpya wa  ccm   aliwahakikishia  wajumbe  hao kuwa     atahakikisha   anafanya  kazi ya  kuimarisha   chama  hicho  pasipo  kuwa na  ubaguzi wowote na  muda wote   atakuwa  yuko  tayari kwa  ajiri ya kusikiliza  kuro za watu na kuzipatia ufumbuzi wake .
Mkoa wa   Katavi  ambao ulianzishwa  mwaka 2012   hivyo   Beda  Katani  amekuwa ni  mwenyekiti wa  pili wa  chama  hicho    toka   Mkoa wa  Katavi   ulipoanzishwa   Mwenyekiti wa  kwanza   alikuwa ni  Mselemu  Abdala  ambae kwenye uchaguzi huu  hakugombea.
MWISHO

 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa