Home » » MIMBA ZA UTOTONI BADO NI TISHIO KUBWA KATIKA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI

MIMBA ZA UTOTONI BADO NI TISHIO KUBWA KATIKA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



MIMBA za utotoni bado ni tishio kubwa  katika Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ambako wasichana  624 walio na umri  wa chini ya miaka 18 wamejifungua   katika  Vituo vya   Afya  vilivyopo katika  manispaa hiyo .

 Hayo yalisemwa  hapo  jana  na Mkuu wa  Mkoa wa  Katavi    Meja  Generali  mstaafu   Raphael  Muhuga,  wakati wa  uzinduzi  wa  kampeni  ya  siku  16 za kupinga ukatili  wa  kijinsia   zilizofanyika kimkoa   katika  viwanja  vya  Saba Saba kijijini Kabungu  Wilayani  Tanganyika .


Muhuga   alisema  taarifa   kutoka  katika  vituo vya  afya  vya Manispaa ya  Mpanda  ya kipindi cha mwaka jana wa 2016   inaonyesha  kuwa  wasichana 624 wenye  umri wa chini ya  miaka 18 walijifungua  katika  vituo   vya  Afya   vilivyopo  katika  manispaa  hiyo kwamba kiwango hicho ni kikubwa na tishio ..

Alisma   hari  hiyo ya  mimba za utotoni  imekuwa ikifanya    watu wanao tembea   barabarani     au  kwenye  masoko ya  Manispaa ya    Mpanda kukutana na  watoto  ambao wamezaa wakiwa na umri mdogo  huku  mgongoni wakiwa wamebeba watoto wenzao.

 Alifafanua  alisema  utafiti  wa  afya  ya uzazi  na  mtoto  na  viashiria  vya  maralia   wa mwaka   2015 na  2016 uliofanywa  na Ofisi ya  Taifa ya   Takwimu NBS  kwa  kushirikiana  na   Wizara  ya  Afya ,   Maendeleo  ya   Jamii, Jinsia,  Wazee na  Watoto kwa  Tanzania  umeonyesha  mkoa wa  Katavi  ujaongoza kitaifa kwa mimba za utotoni.

Aliongeza kuwa utafiti  huo  umeonyesha  kuwa  kitaifa  asilimia 27 ya  wasichana  wa   miaka   15   hadi 19 wameishaanza  uzazi  asilimia 21 walikuwa wameisha zaa  mtoto hai angalau mmoja   huku katika  mkoa wa   Katavi   asilimia  45 ya   wasichana  wa   miaka 15   hadi  19 wameisha    anza  uzazi ,ambapo asilimia 33.3 wakiwa  wameshazaa mtoto  hai   angalau  mmoja. .

Kuhusu    unyanyasaji wa  kijinsia  Muhuga lisema kuwa i  jumla ya  kesi  1,178 zililipotiwa  katika   vituo  vya kutolea  huduma  za   afya  mkoani humo na maofisa ustawi wa jamii katika mwaka   2016.

Muhuga  alisema   kati  ya  kesi  hizo  401 zilihusu ukatili wa  kimwili , kesi 66 zilihusu  ukatili wa  kingono ,kesi  264 zilihusu  ukatili  wa    kisaikolojia  na  kesi  447 zilihusu kutelekezwa watoto na familia zao kwamba  wa ukatili wa kimwili  au  ngono  ulifanywa na wanaume .

Kwa upande wake  Mkuu wa  Wilaya ya   Mpanda    Liliani   Matinga   aliwataka   wanawake    ambao  wanatabia ya kupiga waume zao  waache  tabia   hiyo mara moja kwamba inawaaibisha wanawake wote nchini ..


Nae  Kamanda wa  Polisi wa   Mkoa  wa  Katavi  Damas  Nyanda     alieleza    licha  ya   jitihada   zinazochukuliwa  na  Serikali  kwa kushirikiana  na  makundi  mbalimbali  ya kijamii  ,takwimu   bado  ninaonnnyesha  ongezeko  la ukatili  wa kijinsia .
Alisema  ongezeko hilo  linachangiwa  na  changamoto zifuatazo    ambazo ni  imani za kishirikina ,mila  na desturi  za  badhi ya makabila ,umasikini ,  elimu na ukosefu wa  nyumba  salama   ambapo  baadhi ya wazazi  wamekuwa wakiwalaza wageni wao na  watoto wao na kusababisha  wageni hao kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa