Home » » KATEKISTA AFA BAADA YA KUONGOZA IBADA YA MAZISHI.

KATEKISTA AFA BAADA YA KUONGOZA IBADA YA MAZISHI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na  Walter   Mguluchuma
   Katavi.

KATEKISTA  wa Kanisa katoliki Jimbo la Mpanda mkoani Katavi aliyekuwa akitoa huduma za kiroho katika Kigango cha Mchakamchaka , Noel Sitemele amefikwa na umauti muda mfupi baada kumaliza kuongoza ibaya ya mazishi ya muumini wake juzi .

Kigango cha Mchakamchaka kipo  kijiji ni Majalila katika Parokia ya Mpanda Ndogo katika wilaya ya Tanganyika mkoani humo.

Akisimulia tukio hilo  Diwani wa  Kata ya   Mpanda  ndogo Hamad  Mapendo ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.

alisema  mwalimu huyo wa dini  pia   alikuwa  Mwenyekiti wa   Kijiji cha   Majalila   Halmashauri ya   Mpanda   Wilaya ya   Tanganyika .

  Alisema katekista huyo alifariki dunia juzi   juzi , saa kumi na  moja  jioni muda  mfupi baada ya kufikishwa   katika   zahanati ya  Kijiji     hicho   kabla  hata ya kuanza kupatiwa matibabu.

 Alisema  kabla ya mauti  hayaja  mfika  siku  hiyo  marehemu   aliongoza ibada ya  mazishi  kuanzia  mwanzo wa  ibada   hadi mwisho wa ibada ya mama   mmoja   ambae   alikuwa   amefariki dunia  kwenye  kigango hicho  siku  hiyo.

Mapengo   alieleza   mara   baada ya   kumaliza   mazishi ya mama huyo   muda  mfupi uliofuata  alianza  kujisikia  vibaya kiafya  hari    ambayo ilimfanya    aamue  kurudi  nyumbani  kwake na kuwaacha waombolezaji  wengine waliokuwepo  kwenye  msiba huo.

Baada ya kuwa  amefika  nyumbani  kwake  hali yake   ilizidi kubadilika  ambapo aliomba    msaada  kwa  majirani zake wa  kupelekwa  kwenye   zahanati ya   kijiji  hicho   ambayo haiku mbali kutoka nyumbani kwake .
.
Alisema marehemu  huo  alifikishwa  kwene  zahanati ya   kijiji   cha  Mchakamchaka ambapo   wakati  tabibu   akiwa   anataka kuanza  kumpatia   huduma   akawa   amefariki dunia na kusababisha simanzi na mshtuko  mkubwa  kwa  waliokuwa wamemzindikiza .

  Taarifa  za  kifo cha  Katekista  huyo   ziliwafikia  waombolezaji  walikuwepo kwenye   msiba wa  marehemu   ambae   alikuwa  ametoka   muda  si  mrefu   kuongoza  ibada ya  mazishi hari   ambayo iliwafanya  waombolezaji  wengine  washindwe  kuamini  kama  kweli  katekista  huyo    aliyeongoza  mazishi  kama  kweli   amefariki dunia .

Maziko ya  Katekista   huyo yalifanyika   jana  katika   makaburi ya   Mchakamchaka ambapo   ibada ya  mazishi iliongozwa  na  Padri  Pascal  Kipenye  ambae ni   Paroko wa  Parokia ya  Mpanda   Ndogo  yalihudhuriwa  pia   na   Mbunge wa  Jimbo la   Mpanda   Vijijini Moshi  Kakoso

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa