Home » » TAWA INATAMBUA UHIFADHI HAUWEZI KUPATIKANA BILA KUWEPO UTULIVU KWENYE MAENEO YA HIFADHI.

TAWA INATAMBUA UHIFADHI HAUWEZI KUPATIKANA BILA KUWEPO UTULIVU KWENYE MAENEO YA HIFADHI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma .
      Katavi .
Mamlaka ya usimamizi wa   Wanyama  pori  Tanzania  TAWA     inatambua kuwa   mafanikio  ya uhifadhi   hapa  Nchini   hayawezi  kupatikana  bila  kuwepo  utulivu  kwenye maeneo  ya hifadhi  kutona  na ujangili ,uvamizi  wa  maeneo  ya  uhifadhi  hivyo    TAWA   itaendelea  kuimarisha  uwezo wa  ndani  katika  kupambana na   ujangili  na kudhibiti  uvamizi wa  mifugo  na kilimo  kwenye maeneo  ya mapori ya akiba na tengufu.
  Kauli hiyo  ilitolewa  hapo  jana  na  Kaimu   Mkurugenzi  Mkuu  wa  TAWA  Dkt   James  Mwakibara  wakati  wa kufunga  mafunzo  ya  jeshi usu   kwa  Maafisa  59 wa kutoka   TAWA  yaliokuwa  yakifanyika  kwenye kituo  cha  mafunzo cha  Mlele   Mkoani   Katavi .
 Alieleza  lengo kubwa  la  mafunzo  hayo  ni kuwaandaa  watumishi  wa  TAWA  kufanya kazi  katika  mfumo  wa  kijeshi   PARAMILITARY  ili  kuboresha  utendaji  kazi  kwa kujifunza  mbinu  za kupambana  na ujangili ,kuimarisha  nidhamu  ya watumishi  na kuboresha  mtiririko  wa kutoa na  kupokea amri.
 Alisema   katika  swala  nzima la  kuapambana  na  ujangili  hapa   nchini   TAWA  inaendelea  kushirikiana  na Taasisi   za  uhifadhi  na  vyombo vya  dola  pamoja na  wananchi  katika  kupambana  na ujangili.
  Alieleza  kuwa   wanaelewa   jitihada   zinazofanywa na     Bodi ya   Mamlaka  hiyo  za kuhakikisha  wanapata   zana  za kufanyia  kazi  ikiwemo  kupata  sheria  ya  Mamlaka  na   Strategic  plan itakayo saidia   kuwapa  nguvu  katika kutekeleza   kazi zao.
  Dkt   Mwakibara  alisema   TAWA  ni   Shirika  kubwa  na limetapakaa  Nchi  nzima  inamiliki  maeneo ya  wanyama pori  makubwa  mara  mbili  zaidi  ya  TANAPA   na  mara 13  zaidi   Mamlaka  ya  hifadhi  ya  Ngorongoro  NCAA.
Ukubwa  wa  eneo   hilo ni   mtaji  katika  uchumi  na uzalishaji  ili kufikia  malengo  yaliowekwa  wanapaswa kuwa wabunifu  kwenye  kuongeza  mapato  na kudhibiti  mianya  ya upotevu wa  mapato ya   Nchi .
Alifafanua kuwa   katika  mwaka  wa  fedha    wa  2016 na 207  Mamlaka  ilipanga kukusanya  jumala ya  shilingi   Bilioni  40   lakini  zilikusanywa   shilingi  Bilioni 36  kwa  hiyo ni  jukumu  lao   wote  kuhakikisha  wanapandisha  mapato  ili  kuweza  kutimiza  malengo  na kuweza kutatua changamoto  za uhaba  wa vitendea kazi  na kuboresha miundo mbinu.
Nae Mwenyekiti  wa  Bodi ya   Wakurugenzi  ya   Mamlaka  ya usimamizi wa  Wanyama  Pori  Tanzania    TAWA     Meja  Generali   Mstaafu    Hamis    Semfuko    alieleza  kuwa ni  mategemeo yake  kuwa  mafunzo  walipatiwa  maafisa hao wa  Kati wa  TAWA   yatawaongezea  nguvu  katika kupambana na  ujangili  na  changamoto nyingine  ikiwemo  matumizi  ya silaha za  kivita  katika ujangili  na uvamizi wa maeneo ya  hifadhi.
 Alisema katika kuboresha  ulinzi wa  rasilimali za  nchi  katika  maeneo yaliochini     Bodi  ya  Tawa ilisha  towa    agizo  kwa  Manejimenti  kuhakikisha  kwamba  Ofisi zote  za wakuu  wa vituo  zinahamia  kwenye  maeneo ya  mapori  husika   badala ya kuwa     mijini .
Mwakilishi wa  Mkurugenzi  Mkuu wa   Tanapa   ambae    ni   Mkuu wa   Hifadhi ya   Taifa ya   Katavi     Izumbe     Msindai   aliwaka  watumishi  wanofanya kazi  kwenye   Hifadhi  na   mapori ya   akiba    pamoja na tengefu  waepuke  kujihusisha na  maswala ya  Rushwa  kwani  wapo  baadhi  mwa  wtumishi wamekuwa sio  waaminifu  .
Mkufunzi   Mkuu wa   mafunzo  hayo  Mhifadhi    Fidelis   Kapalata   alisema   wahitimu  hao  wamepatiwa  mafunzo hayo kwa  muda wa     wiki   sita   na  yamewajengea  utimamu  wa  mwili  na mbinu  za  kupambana  ujangiri pia  ujasiri  wa kujiamini  na  hari  katika kulinda  rasilimaii za  wanyama .


DD

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa