Home » » MDOGO WAKE PINDA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCM WA WILAYA

MDOGO WAKE PINDA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCM WA WILAYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter   Mguluchuma .
        Katavi .
Chama  cha  Mapinduzi  CCM    Wilaya ya  Mlele  Mkoani   Katavi   kimefanya  uchaguzi wa  ngazi ya  Wilaya  na kuwapata  viongozi wa  Chama  hicho watakao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo huku    Walfugang  Mizengo  Pinda  ambae  ni  mdogo wake na  Waziri  Mkuu   Mstaafu  Mizengo  Pinda   akichaguliwa kuwa    Mwenyekiti wa  CCM   wa  Wilaya  hiyo .
  Uchaguzi huo ulifanyika  juzi   katika  ukumbi wa  Chama  cha   Msingi     Ukonongo ulipo     Inyonga  Wilayani  Mlele  na  mgeni rasmi  kwenye  Mkutano huo   alikuwa ni    Waziri  mteule wa  Wzira ya   Maji   Eng  Izack    Kamwelwe   ambae pia ni  Mbunge wa  Jimbo la  Katavi .
Katika   hotuba  yake ya ufunguzi wa  Mkutano huo wa   Uchaguzi   msimamizi  huyo wa  uchaguzi aliwaasa wajumbe wa mkutano huo kujiepusha na  kuwachagua viongozi watakao washawishi wawachangue kwa  ajiri ya kuwapatia  rushwa .
Akitangaza  matokea  hayo ya uchaguzi     msimamizi wa uchaguzi huo   Katibu   Mwenezi wa   CCM  wa   Mkoa wa   Katavi    Joseph  Makumbule alisema   idadi ya wajumbe waliotakiwa kupiga kura  541 ambao walikuwa wametoka   kwenye   Kata  15 za   Wilaya  hiyo  lakinii  waliohudhuria ni wajumbe  477.
Makumbule  alifafanua kuwa  wagombea walikuwa ni watatu  kwenye   nafasi ya    Mwenyekiti  ambapo kura  zilizopigwa  zilikuwa ni 477    ambapo kura moja iliharibika  na  matokeo yalikuwa ni   Gerald  Kasela  alipata kura  146   John  Mbogo  kura  110 na  Walfffugang  Mizengo  Pinda kura  220.
Kwa  mujibu  wa   Kanuni   mshindi wa  nafasi  hiyo   lazima  avuke  nusu ya kura   hivyo  wajumbe wa  mkutano huo walilazimile wapige kura  kwa  mara ya pili kwa wagombea  wawili walipata kura za juu  ambao ni   Gerald   Kasela  na   Walfugang  Mizengo  Pinda .
  Ambapo katika uchaguzi huo wa marudio  kura  450  zilipigwa   ambapo   Gerald  Kasela   alipata kura  156  na   Walfugang  Mizengo  Pinda  alipata kura  280 na kura   8 ziliharibika   hivyo   msimamizi wa  uchaguzi   Joseph  Makumbule  alimtangaza   Walfugang   Mizengo  Pinda kuwa  ndio   mshindi w   nafasi  hiyo   na   alimtangaza rasmi kuwa   Mwenyekiti wa  Wilaya wa  CCM  wa  Wilaya ya  Mlele.
 Pia        mkutano huo ulimchagua   Renatus  Kamaninja kuwa  Katibu   Mwenezi wa  Wilaya     baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu  na   Lachael  Kasanda   ambae ni   Mkuu wa  Wilaya ya   Mlele  alichaguliwa kuwa   mjumbe wa   mkutano mkuu wa    CCM  Taifa   baada ya kuwashinda wagombea  tisa wa  nafasi hiyo .
  Na  kwa  upande wa   Wilaya ya  Mpanda   Abal   Hamis   Kimanzi   alchaguliwa  kuwa  Mwenyekiti wa   Wilaya   hiyo  baada ya kuwashinda   Method  Mtepa  na  Wense   Kaputa waliogombea  nafasi  hiyo kwenye    uchaguzi uliofanyika   katika   Uwanja wa  Mpira wa  Azimio  Mjini  hapa.
Nafasi ya    Katibu  Mwenezi wa   Wilaya ya   Mpanda    alichaguliwa   Elias   Milwano   ambae   aliwashinda  wagombea   wawili waliokuwa  wameomba   nafasi  hiyo .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa