Home » » WAZAZI WALAUMIWA KWA KUMWOZA MTOTO WAO BUBU MWENYE MIAKA 13.

WAZAZI WALAUMIWA KWA KUMWOZA MTOTO WAO BUBU MWENYE MIAKA 13.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma.
         Katavi

WAZAZI  wa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 ambae ni mlemavu wa kusikia  na kusema ‘bubu kiziwi “ wanadaiwa  kumuozesha  kwa nguvu  kwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 18 imeinika  .
Wazazi hao na wanandoa hao wote wanaishi katika kijiji cha Masigo  kilichopo  katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi .
Mratibu wa Marie Stopes mkoa wa Katavi , Seif Kajiko amelaani kitendo hicho chs wazazi  hao  kumuozesha  mtoto wao huyo wa kike  kwa nguvu akidai  kunasababishsa kuongezeka kwa mimba za utotoni  mkoani humo .
Kajiko alilaani tabia hiyo wakati wa maadhimisho ya tamasha  la vijana  lililojumiisha wanafunzi kutoka shule  kumi za sekondari za Manispaa ya Mpanda  lililoandaliwa na Marie Stopes  kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Katavi ambapo yalifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini hapa .
Aliiasa jamii mkoani humo kuachana na tabia  hiyo ya kuwaozesha binti zao wenye umri mdogo  kwa kuwa madhara yake ni makubwa  ikiwemo vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na matatizo ya uzazi .
  Alisisitiza kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Marie Stopes kukabiliana na mimba za utotoni kwa kutoa  elimu shuleni bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo baadhi ya waliku wa shule za sekondari  kukataa kutolewa kwa elimu ya uzazi wa mpango kwa wanafunzi wa kike .
Kwa upande wake Mratribu wa Vijana wa Marie Stopes  nchini , Daniel Mjema lengo la tamasha hilo ni kutoa elimu ya afya ya msingi kwa vijana elimu  ya uzazi wa mpango na jinsi ya kujikinga na maabukizi ya VVU na Ukimwi .
Nae Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi , Wilbroad Marandu aliwaasa wanaume  wote moani humo  kushirikiana bega kwa began a wenza wao  na kujitokeza  kupata  elimu  ya  uzazi wa mpango .
“Baadhi ya wanaume wana tabia ya kuwazuia wake zao  kujiunga na uzazi wa mpango kwa kisingizio kuwa mwanamke ni wa kuzaa tu hadi mayai yake  ya uzazi ya muishie “ alisisitiza
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Sekinari ya Wasichana Mpanda alidai kuwa mimba na ndoa za za utotoni zinamkwamisha mtoto wa kike kutimiza ndoto zake .
Mwisho




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa