Home » » KAYA ZAIDI YA 80 WALAZIMIKA KULALA NJE

KAYA ZAIDI YA 80 WALAZIMIKA KULALA NJE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mpanda
KAYA zaidi ya 80  kutoka kitongoji cha Kitupa wilayani Mlele  katika mkoa wa Katavi hawana makazi ya kudumua  na kulazimika kulala  nje usiku baada ya nyumba zao kubomolewa  ili kupisha upanuzi wa eneo la mnada .

Baadhi yao wameleza kuwa  nyumba zao  zilibomolewa juzi saa sita mchana na askari wa Hifadhi  za Taifa (Tanapa)  wakishirikiana na  askari wa jeshi la akiba maarufu mgambo  ambapo sasa  wanalazimika  kulala nje na wake zao karibu na watoto  na wakwe zao  ikiwa ni kinyumbe na mila na dessturi zao .

Mkazi wa kitongoji hicho , Eliasa Chimbamawe alidai kuwa wazazi wake walijenga na kuishi hapo tangu mwaka 1949  hadi walipoaga dunia mwaka 1975  na kuzikwa hapo .

Nae Festo Lazaro alieleza kuwa yeye na familia yake  walilazimishwa  kubomoa  nyumba yao na askari hao  huku akiamriwa kuimba nyimbo  za hamasa ili wasichoke .

Kwa upande  wake Anoneta Joseph ambaye ni mjane alidai kuwa  nusura watoto wake watatu wapoteze maisha  ambapo walizimia  baada ya kuelezwa na wenzao kuwa  nyumba yao imebomolewa  na askari .

Meda Shigela aliyedai kuwa ana watoto 13 alijenga na kuanza kuishi hapo tanguj 1997 ambapo  sasa amelazimika kulala nje usiku  na mke wake , watoto  na wakwe zake  ikiwa ni kinyume na desturi na mila zao .

  Mpelwa \John alidai kuwa  mbaya zaidi  licha ya nyumba zao  kubomolewa  pia vyoo vimetekelezwa na sasa  wanalazimika  kujisaidia  porini  huku wakihofia  kulipuka kwa magonjwa  ya kuhara ikiwemno  kipindupindu.
Mwenyekiti  wa  Kitongoji  hicho   cha   Kitupa Mkamba Mzoloka  alidai kuwa  wakazi wake  wanateseka kwa  kukosa  makazi ya kudumu  ambapo  walibomolewa nyumba zao  bila kutaarifiwa kwanza .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa