Home » » Vyeti feki vyaathiri huduma Duka la MSD

Vyeti feki vyaathiri huduma Duka la MSD

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



*Lashindwa kufanya kazi saa 24
*Matarajio ya wananchi yatoweka
NA WALTER MGULUCHUMA, Katavi
ILIKUWA ni Jumanne ya Januari 17 mwaka huu pale wananchi wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla walipoyaona mapambazuko ya aina yake katika sekta na huduma ya afya.
Sekta hii muhimu katika maendeleo ya taifa, kwa miaka mingi imekuwa ikikumbana na changamoto kadhaa karibu kila kona ya Tanzania, kubwa ikiwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.
Jumanne hiyo ya kukumbukwa ndio siku ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozindua duka la serikali linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) lililopo  katika Hopitali ya Manispaa ya  Mpanda  ambayo ndio inayotumika kama  Hospitali ya Mkoa wa Katavi.
Wananchi waliohudhuria hafla hiyo waliifurahia hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba mbali na uhaba wa dawa na vifaa tiba kwa mikoa iliyopo pembezoni mwa Tanzania, Katavi ni mmojawapo, tatizo jingine ni ukubwa wa bei za dawa.
“Hili duka la serikali litatuuzia dawa kwa bei tunayoimudu wengi tofauti na maduka ya wafanyabiashara wengine,” alisikika akisema kwa matumaini makubwa mmoja wa wananchi waliokuwapo siku hiyo.
Huenda matarajio na matamanio hayo yakawa yameanza kufifia ndani ya miezi minne tu tangu kufunguliwa kwa duka hilo. Ni nini sababu ya kupungua kwa matumaini hayo?
Serikali ya Awamu ya Tano kwa nia njema kabisa, inaendelea na ukaguzi na ufuatiliaji wa vyeti vya kitaaluma kwa wafanyakazi wake kwenye sekta mbalimbali, ikiwamo pia hii sekta nyeti ya afya.
“Hii ni hospitali kubwa mkoani Katavi; ndio kimbilio letu na haistahili kukosa dawa na vifaa tiba hata vile vya msingi kabisa, lakini bahati mbaya hata bada ya kuwapo kwa dula la MSD, bado tunalazimika kununua dawa kwa wafanyabiashara,” anasema Said Juma, Mkazi wa Kawajense mjini hapa.
Juma anasema Duka la MSD nalo lina matatizo yale yale yaliyopo hospitalini hapo; halina dawa muhimu kwa magonjwa ya kawaida kabisa kwa wakazi wa Mpanda!
“Shida inakuwa kubwa zaidi nyakati za usiku kwani maduka mengi ya dawa huwa yamefungwa. Kimbilio letu huwa ni Duka la Dawa la Mkasu lililo jirani na hospitali. Hapo kila alfajiri utakuta watu walikuwa wakihitaji huduma tangu usiku wa manane, wakisubiri lifunguliwe,” anasema na kuongeza kuwa aghalabu nalo huwa halina baadhi ya dawa walizoandikiwa wagonjwa wengi.
Kukosekana kwa dawa jirani na hospitali, kwa upande mwingine, ni neema kwa waendesha bodaboda wenye kijiwe karibu na Hospitali ya  Mkoa na mmoja wao anasema:
“Watu wengi huwa na haraka ya kununua dawa mbali na hospitali, maeneo ya mjini. Hawa lazima wakodi bodaboda. Hii ndio huduma yetu kwa wananchi na kwetu sisi ni kazi pia.”
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo, iliahidiwa kuwa lingefanyakazi saa 24 likiwahudumia wakazi wa Mpanda na mikoa ya jirani.
“Duka hili litamaliza tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali hii, vituo vya afya na zahanati za Mkoa wa Katavi. Serikali ina mikakati ya kufungua maduka ya dawa kupitia  MSD kwenye kila mkoa hapa nchini  ili kuondoa  tatizo la vifaa tiba na dawa na kuwapunguzia  wananchi gharama za matibabu,” alisema Majaliwa.
Lakini sasa duka hilo hufanyakazi kwa saa kadhaa tu kwa kuwa hulazimika kufungwa nyakati za usiku kutokana na uhaba wa wafanyakazi.
Walau wafamasia watatu waliokuwa wakihuduma dukani hapo wamekumbwa na zoazoa ya vyeti feki na hivyo kuathiri huduma za duka hilo na kuongeza matatizo zaidi juu ya upungufu uliopo wa dawa dukani hapo.
Wakati wa uzinduzi Januari mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurent Bwanakunu, lengo la kufungua maduka katika mikoa saba nchini ni kusogeza   huduma karibu na wananchi waweze kupata dawa bora na kwa bei nafuu.
Hata hivyo, ahadi hizo za Waziri Mkuu na  Mkurugenzi wa MSD hazijafanikiwa kutatua tatizo la upungufu wa dawa mkoani Katavi.
Kwni  mpaka sasa  dawa  nyingi zimekuwa zikinunuliwa na wananchi kwenye  maduka ya Wafanya biahara wa mitaani kutokana na  duka  hilo la MSD  kutokuwa na  dawa  zenye  mahitaji kwa wananchi.
Baadhi ya  wananchi wameanza kuingiwa na  mashaka kuwa  huenda  ndani zinazoletwa  hapo   ni  zile   ambazo sio  mahitaji kwa  wakazi wa   Mkoa wa  Katavi .
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa