Home » » MWENYEKITI WA CCM TAWI LA ITENKA AUWA KIKATILI KWA KUKATWA NA MAPANGA

MWENYEKITI WA CCM TAWI LA ITENKA AUWA KIKATILI KWA KUKATWA NA MAPANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
.
 Walter  Mguluchuma .
  Na  Arine  Temu .
  Katavi.
  Mwenyekiti wa  CCM   wa    Tawi  la   Itenka      katika  Kata ya  Itenka   B Tarafa  ya  Nsimbo  Wilaya ya  Mpanda   Mkoani  Katavi  Hapiam   Salvatory  50  ameuwawa kikatili kwa kuchalangwa kwa  mapanga  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili wake  na kutenganishwa na  kiwili wili.
Kwa  mujibu wa  Kamanda wa  Jeshi  la  Polisi wa  Mkoa w  Katavi  Damas  Nyanda   aliwaeleza  wandishi wa   Habari  kuwa tukio  hilo la mauwji ya kikatili lilitokea  hapo jana  majira ya saa  saba  mchana .
  Alisema   kuwa  siku  hiyo ya tukio  marehemu  aliaga nyumbani  kwake kuwa   anakwenda  mtoni  kwenye   shughuli  zake  alizokuwa  akifanya kila  siku  za kuvua samaki  kwenye mto Itenka  uliopo   Kijijini hapo .
  Wakati  akiwa njiani kuelekea  mtoni   marehemu  alivamiwa na watu  ambao walikuwa na  mapanga  na kumkatakata   katika  sehemu mbalimbali za  mwili wake  na kuutenganisha  kiwili wili  na  kichwa   hadi kufariki  Dunia hapo hapo .
  Kamanda   Nyanda   alieleza  kuwa  baada ya   wauwaji  hao  kufanya  mauwaji ya kikatili na yakusikitisha  waliondoka na kutokomea kusiko  julikana  na kuuwacha  mwili wa  Mwenyekiti huyo wa  CCM  ukiwa  unagalagala   barabarani .
   Mwili wa  marehemu  huyo  ulionwa  na  wananchi  wawili  ambao wakuwa wakipita  kwenye  eneo  hilo  na  ndipo walipokwenda kutowa taarifa kwa  uongozi wa  Kijiji  ambao nao walitowa  taarifa  kw  jeshi la   Polisi  ambao walifika  kwenye  eneo hilo  huku wakiongozwa na  yeye   Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa  Katavi  na   walikuta mwili wa  marehemu  huyo ukiwa umelazwa  barabarani  huku  akiwa ameuwawa  kikatili kwa kukatwa na  mapanga.
  Kamanda   Nyanda  alisema  kabla ya tukio  hilo   marehemu  huyo  aliwahi kuandikiwa  barua   mbili miaka   miwili  iliyopita ya kutishiwa kuuwa na watu wasio  julikana walikuwa wakimtuhumu kuwa ni  mchawi .
  Alieleza  kuwa  katika  tukio  hilo  watu  watatu  wanashikiliwa na  jeshi la  Polisi kwa tuhuma za  mauwaji  hayo ya  mwenyekiti wa  CCM  na  wanaendelea kuhojiwa kwa  mahijiano  zaidi .
Kamanda   Damas  Nyanda   ametowa  wito kwa  wananchi wa   Mkoa  wa  Katavi  kuacha  tabia ya kujichukulia  sheria  mikononi  kwani kufanya  hivyo ni  kosa  la jinai .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa