Home » » WILAYA YA TANGANYIKA KUANZISHA UTALII WA ASILI

WILAYA YA TANGANYIKA KUANZISHA UTALII WA ASILI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 










Walter  Mguluchuma .
       Katavi .
   Halmashauri ya  Wilaya ya   Mpanda    Katika    Wilaya   Mpya   ya    Mkoani   Katavi   imepanga kua  .
  na    Utalii  wa   Asili  ili   kuweza kuwavutia watalii  mbalimbali wa   nje  ya   Nchi  na   ndani  ya  Nchi na kuwaongezea  wananchi  kipato  chao .
  Hayo  yalisemwa  hapo  juzi  na  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Tanganyika   Salehe   Mhando     wakati   alipokuwa  akiwa  wahutubia    wananchi wa  Kijiji  cha    Vikonge   Tarafa ya  Kabungu  kwenye  mkutano wa  hadhara  uliofanyika   Kijijini  hapo .
  Alisema     Wilaya  ya   Tanganyika   inaomstu mkubwa  wa  Tongwe  ambao upo  kwenye  Kijiji  cha  Vikonge    ambao  una    wanyama  wengi     aina  ya  Sokwe  kuliko   wanaopatikana  sehemu  nyingine  yoyote ile   idadi  kubwa  kama  hiyo .
  Hivyo  pamoja  na  kuwepo kwa  idadi  kubwa ya  Sokwe wanaokadiliwa kuwa  zaidi ya  3000  bado  watu  wengi wa   nje ya  nchi  na  ndani ya   nchi  hawajafahamu  uwepo wa  sokwe  hao  katika   Wilaya ya  Tanganyika .
  Hivyo  ilikuweza  kuwafanya   watalii   wawe  wanafika  Wilayani   Tanganyika  kwa  ajiri ya kuona  Sokwe  hao  wamepanga kuanzisha  utalii  wa  asili  ambapo  mambo  mengi ya kiasili ya  Mkoa wa  Katavi  yatakuwa  yanaonyeshwa.
Mhando   alieleza  miongoni  mwa  mambo yatakayokuwa  kuwa  yanapatikana  kwenye  utalii huo wa  asili  ni  mambo ya     ngoma  za   asili  za   Mkoa  wa   Katavi .
  Hivyo   aliwataka   wanachi wa  Wilaya  hiyo  kujiandaa  na kutumia  furusa  hiyo  vizuri  ili   kuweza  kujiongezea   vipato  vyao ambavyo vitawasaidia  kuboresha  maisha  yao .
Afisa  Maliasili  wa  Halmashauri   hiyo  Josephina   Rupia    alisema   utalii wa  Kiasili  umepangwa kuwa  utakuwa unafanyika  katika   Kijiji  cha  Vikonge na  jamii  kama  jamii  itanufaika  na  utalii  huo .
   Hivyo  aliwataka  wakazi wa  Kijiji  hicho  kuwa  tayari kuupokea  mpango  huo wa kuanzisha  utalii wa kiasili kwa manufaa yao na  kw  manufaa ya  watu wa   Mkoa wa   Katavi na  Taifa kwa  jumla .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa