Home » » MIAKA MINNE JELA KWA KUKUTWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA

MIAKA MINNE JELA KWA KUKUTWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na   Walter  Mguluchuma
  Katavi

MAHAKAMA  ya  Wilaya ya Mlele iliypo katika mkoa wa Katavi
imemuhukumu mkazi wa kijiji cha Tupido Ephance Seleman (42) kutumikia
miaka minne jela  baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili kwa
kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kinyume cha
sheria .

Aidha mshtakiwa  huyo alitiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kukutwa na
lita tisa za pombe haramu maarufu ‘gongo’  baada ya kukiri kutenda
makosa hayo mawili huku akisema kuwa sare hiyo ya JWTZ alimnyang’anya
mtu mmoja aliyekunywa pombe hiyo haramu nyumbani kwake  na kushindwa
kumlipa.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo  jana kwa mara ya kwanza
ambapo alikiri kutenda makosa hayo mawili baada ya kusomewa  mashataka
yake ..

“Nakiri kufanya makosa hayo  lakini sare ya JWTZ nilimnyang’anya mteja
wangu aliyekunywa  pombe  aina ya gongo  iliyopikwa nyumbani kwangu
baada ya kushindwa  kunilipa “ alieleza

Hakimu wa mahakama hiyo ,Teotimus Swai licha ya mshtakiwa huyo  kukiri
makosa yake amempatia adhabu hiyo kali  ili iwe fundisho kwa wengine
wenye tabia kama zake.

Awali Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi wa Polisi , Baraka Hongoli alisema
kuwa mshtakiwa huyo alitenda makosa hayo Januari , 29, mwaka huu,

Alisema siku hiyoya tukio askari polisi walipekuwa nyumba yake
kufuatia taarifa kuwa ni kinara wa kupika na kuuza pombe hiyo haramu
ndipo walipomkuta akiwa na sare moja ya JWTZ.

Mwendesha Mashtaka huyo aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali dhidi
ya mshtakiwa huyo  ili iwe fundhisho  kwa watu wengine ambao wamekuwa
wakimiliki sare za kijeshi kinyume cha sheria  na kufanya uhalifu
wakiwa wamezivaa  na kuchafua sifa ya jeshi hilo .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa