Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga na Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Matheo Singimwa jana waliongoza maelfu ya Wakazi wa Manifaa ya Mji wa Mpanda Mkoani Katavi . katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Singida Kamishina msaidizi mwandamizi Peter Kakamba .
Mazishi hayo yaliohudhuriwa na maelfu ya Wakazi wa Manispaa ya Mpanda yalifanyika jana katika makaburi ya Kasimba katika manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi .
Kamanda Kakamba alifariki Novemba 29 huko katia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoana na tatizo la ugonjwa wa tumbo na uluopekea kufanyiwa upasuaji kabla ya kifo hicho .
Akisoma wasifu wa Marehemu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alieleza kuwa marehemu Kakamba alizaliwa June mwaka 1963 katika Kijiji cha Kawajense manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi .
Katika uhai wake marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika jeshi la Polisi alizija nyadhifa hizo kuwa aliwahi kuwa OCD Wilaya ya Mafinga, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida .
Mkuu wa Mkoa wa Singida Eng Matheo Singimwa alimwelezea marehekumu kuwa ameacha pengo kubwa katika Mkoa wa Singida kutokana na mikakati waliokuwa wameipanga ya kuimalisha ulinzi .
Alisema kutoka na uchungu aliokuwa nao yeye Mkuu wa Mkoa wa Singida kutoka na kifo cha Kamanda huyo ambae alihamia mkoani hapo miezi mine iliyopita ndiomaana alishindwa kutowa hutuba hapo juzi Mkoani Singida walipokuwa wakiaga mwili wa marehemu kabla ya kuusafirisha Mkoani Katavi .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga alieleza kuwa marehemu alikuwa ni mwadilifu na ndio maana aliweza kufikia cheo cha Kamishina msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi .
Alisema kifo chake ni pengo kwa Serikali kwani ilikuwa imewekeza kwake ili aendelee kulitumikia Taifa kwa kipindi kirefu .
Kwa upande wake Padri aliyeendesha misha hiyo ya mazishi ambae ni makamu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Pdri Patrick Kasomo katika mahubiri yake alieleza kuwa marehemu alitimiza majukumu yake ya kuwatumikia watu na ndio maana aliweza kufikia ngazi hiyo ya kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa .
Pia aliwataka makamanda wa Polisi kuwa na tabia ya kwenda kusali kwenye makanisa yao na misikitini wanapo kuwa wamemaliza majukumu yao ya kazi kwenye maeneo yao na wasiwe wanawazuia askari wao wa ngazi za chini kwenda kusari .
Alisema wapo baadhi ya Makamanda wa Polisi na ma OCD wamekuwa na tabia ya kuwazuia askari wao kwenda kusari na askari ambao wamekuwa wakienda kusar I wamekuwa wakiwapatia adhabu watambue kuwa kufanya hivyo wanakuwa wanamkosea Mungu .
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Dodoma , Rukwa Katavi na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida na Wakuu wa Wilaya za Uyuwi Mkoani Tabora , Dc wa Sindiga na wa Mpanda.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment