Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anjelina Mabula ameziagiza Halmashauri kuacha tabia ya kuwahamisha watu kwenye Makazi yao wanayoishi kabla ya kuwalipa fidia .
Agizo hilo alilitowa hapo jana kwenye mikutano ya hadhra iliyofanyika katika kata za Misunkumilona Nsemlwa kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata za Nsemlwa na Minsukumilo kwenye mikutano ya hadhara alipokuwa akizungumza na watumishi wa Wizara yake wa Halmashauri za Mpanda , Nsimbo na Manispaa ya Mpanda kwenye kwenye ukumbi wa idara ya Maji mjini hapa .
Alisema kumekuwepo na tabia ya kuwahamisha wananchi kwenye maeneo yao wanayoishi bila kuwalipa fidia na maeneo hayo kupimwa viwanja na kupewa watu wengine .
Alisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano haiiko tayari kuona wananchi wanaondolewa kwenye maeneo yao waliokuwa wakiishi bila kulipwa fidia kwani kufanya hivyo ni kuwanyanyasa wananchi .
Naibu huyo Waziri wa Ardhi alikemea tabia inayofanywa na watumishi wa iIdara ya Ardhi ya kupima maeneo ya viwanja na kuwanyima watu ambao walikuwa wakiishi kwenye maeneo hayo na kuwapatia watu wengine kwani kufanya hivyo ni wizi kwa wananchi .
Hivyo aliagiza kuwa maeneo yote ambayo yatakuwa yanapimwa viwanja wanaotakiwa kupewa kipaumbele ni wale wananchi waliokuwa wakiishi kwenye maeneo hayo baada ya hapo ndipo wepewe watu wengine .
Pia ameziagiza Halmashauri kuhakikisha zinapima viwanja na mashamba kisha kutoa hati miliki za viwanja na kuwapatia wananchi hati hizo ziweze kuwasaidia katika kuomba hata mikopo kwenye taasisi za mabenki.
Pia hati hizo zitasaidia kupunguza migogoro ya watu wanaovamia maeneo ya taasisi za umma.
Na kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea matra kwa mara. Kwenye maeneo mengi hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment