Na Walter Mguluchuma
Katavi
WAKAZI wa Kata ya Nsemlwa iliyoko katika Manispaa ya Mpanda
katika mkoa wa Katavi wanalazimika kulala mapema kutoka na
kushikwa na hofu baada ya milango na kuta za nyumba wanazoishi
kupakwa damu inayodhaniwa kuwa ya binadamu au mnyama
Nyumba za Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nsemlwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa
Nsemlwa ni miongoni mwa nyumba 300 zilizopo katika mitaa yote mitano
ya kata hiyo zinazodaiwa kupakwa damu hiyo.
Akizungumza na gazeti hili Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo , Jumbe Mselwa
alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili ambapo watu
wasiofahamika walipaka nyumba hizo damu na kusababisha hofu kubwa kwa
wakazi wa eneo hilo.
Alisema taarifa za mkasa huo zilifikishwa ofisini kwa ke na
wenyenyeviti wa wa serikali za mitaa mitano ambapo alilazimika
kwenda kuhakikisha na kukuta nyumba hizo zikiwa zimepakwa damu
nje na nyingine ndani.
Jumbe aliitaja mitaa hiyo ambayo nyumba zake zimepakwa damu
kuwa ni pamoja na Mtaa Kichangani , Migazini ,Kilimani
Tulieni na Mtaa wa Nsemlwa ambao ndio unaongozwa kwa nyumba
nyingi kupakwa damu .
‘Nimewataka wakazi wa kata hiyo mara wanaopoona kitu ambacho
sio cha kawaida watoe taarifa mapema kwa uongozi wao wa
mitaa wanayoishi “ alisisitiza .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsemlwa , Adamu Masigati
alikiri kwamba nyumba yake ni miongoni mwa nyumba ambazo
zimepakwa damu usiku huo ambapo n wakazi wa mtaa huo wanahoji
kulikoni tukio hilo litokee usiku badala ya mchana .
Msagati alieleza kuwa jana alitaarifiwa kuwa m wa Mtaa huo
mkazi wa mtaa huo alidondokewa na matone ya damu hiyo wakati
alipokuwa ndani ya nyumba yake akila chakula cha usiku .
Akisimulia mkasa huo mkazi huyo aitwae , Raphael Geoge juzi
akiwa nyumbani kwake saa kumi jioni akila chakula sebuleni
kwake ambapo alipoanza kula tonge la pili la ugali ghafla
aliona matone mawili ya damu yenye ukubwa wa sarafu ya
shilingi 100 yakidondoka alipokuwa amekaa .
Alisema tukio hilo ilimshitua ambapo alimwaita binti yake aitwae
Maliselina Joseph ili nae ashuhidie damu hiyo ambayo
haikufahamika imetoka wapi .
Umati mkubwa wa watu walifurika nyumbani kwa Raphael ambapo
walishtushwa baada ya kushuhudia nzi wakiwa wamerundikana kwenye
matone ya damu hiyo ambapo walitoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya
Mtaa wa Nsemlwa.
Mkewe Raphael aitwaye Judith Joseph ambae wakati wa
tukio hilo hakuwepo nyumbani anasema aliporudi nyumbani saa
moja na nusu usiku alikuta familia yake wakiwa wamekaa kama
wagonjwa.
“ Nimemshauri mume wangu tuhamie kwenye nyumba nyingine lakini
amekataa akisisitiza kuwa ingekuwa ni nyumba ya kupanga angehama
lakini hawezi kwa kuwa ni nyumba yake aliyoijenga mwenyewe ….sasa ni
siku mbili zimepita nimeshindwa kufanya usafi wa nyumba kwa ajili ya
woga isitoshe sasa tunalazimika kulala mapema kabla ya saa mbili
usiku” alieleza.
Kwa upande wake Wasitala Ferusi alisema yeye na familia
yake tangu nyumba yao ilipopakwa damu wamekuwa wakijifungia na
kulala mapema huku akiwazuia watoto wake kutembea hata kwa
majirani .
Alisema kinachostaajabisha wengi damu hiyo imepakwa kwenye kuta ndani
ya nyumba huku milango ikiwa imefungwa usiku
0 comments:
Post a Comment