Na Walter Mguluchuma .
Katavi .
Mahakama ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imemuhukumu Mkazi wa Kijiji cha Ilunde Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Festo Joseph 29 adhabu ya kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na kosa la kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa .
Hukumu hiyo ambayo iliwasisimua watu wengi wa Wilaya ya Mlele ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mlele Theotimus Swai baada ya mshitakiwa kukiri Mahakamani hapo kuwa ni kweli alimlawiti mtoto huyo wa kike.
Awali Mahakamani hapo mwendesha mashitaka mkaguzi wa jeshi la Polisi Baraka Hongoli alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Festo alitenda kosa hilo hapo Novemba 10 katika Kijiji hicho cha Ilunde .
Siku hiyo ya tukio mshitakiwa alifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo na kumdanganya mtoto huyo kuwa baba yake ambae hakuwepo nyumbani nyakati hizo za saa sita mchana kuwa alimtuma akamwonyeshe nyasi alizokata kwa ajiri ya kuenzekea nyumba yao katika moja ya pori Kijijini hapo .
Mwendesha mashitaka Hongoli alidai kuwa baada ya mtoto kukubali kuongozana na Festo hadi katika pori hilo ndipo alimkamata na kumpeleka hadi katika Bani moja la jiko la kukaushia tumbaku ambapo aliingia nae na kisha alimfanyia kitendo hicho cha kumlawiti bila kujari mayowe ya mtoto huyo aliyekuwa akipiga kuomba msaada kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata katika sehemu zake .
Mshitakiwa huyo baada ya kuwa amemfanyia unyama huo wa kumlawiti kisha alimrudisha hadi karibu na nyumbani kwa wazazi wake huku akimtishia kuwa asitowe siri hiyo kwa mtu yeyote Yule vinginevyo akifanya hivyo atamuuwa .
Baada ya kufika nyumbani nyumbani kwao mtoto huyo alianza kulia akilalamika maumivu makali aliyoyapata ndipo wazazi wake walimuuliza analia nini ndipo alipowaeleza yaliomfika huku akimtaja muhusika wa kitendo hicho ambapo mbiu ilipigwa Kijijini hapo na kikosi cha Sungusungu kilianza kazi ya kumsaka kijana huyo Festo kwenye kila kona ya Kijiji na kufanikiwa kumkamata majira ya saa 12 jioni akiwa amejificha porini .
Hongoli aliambia Mahakama mshitakiwa huyo wakati akiwa mikononi mwa Sungusungu walimrejesha Kijijini hapo Festo alikiri kutenda kosa hilo huku akiwaomba wakazi wa Kijiji hicho msamaha hata hivyo wananchi hao hawaku mwachia na walimpeleka hadi kwa Mtendaji wa Kata ambapo alikiri tena kutenda kosa hilo na ndipo alipochukuliwa na kufikishwa kituo cha Polisi Inyonga alikiri kwa maneno na maandishi kuwa alimlawiti mtoto huyo .
Mshitakiwa katika utetezi wake Mahakamani hapo aliiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu kwani katika maisha yake alikuwa hajawahi kutenda kosa kama hilo hata hivyo Hakimu Swai alimukumu kifungo cha maisha jela huku akiongeza kuwa kosa hilo halina adhabu mbadala zaizi ya kifungo cha maisha jela .
0 comments:
Post a Comment